Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022Mfano
Katika somo la leo twaona ya kwamba hata watakatifu na mtume Petro waliweza kuanguka katika dhambi. Tusifikiri kwamba sisi wenye Roho hatuwezi kuanguka. Maana yake si kwamba tuendelee kutenda dhambi. Dawa nzuri ya kuipinga dhambi inapatikana katika 1 Yoh 1:9 inayosema hivi, Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.Tusipoiungama dhambi yetu, twakoma kuwa Wakristo. Kwa hiyo twajua kwamba baada ya kushindana na Paulo, mtume Petro akaungama dhambi yake na kujirekebisha. Fundisho lingine ni kwamba mmoja akianguka huwapotosha wengine.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Septemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wagalatia na Hagai. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/