Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Amani ya MunguMfano

God's Peace

SIKU 3 YA 4

NYUMBA YENYE AMANI

KUONGEA NA MUNGU
Muombe Mungu msamaha kama umeumiza hisia za mtu katika familia yako au umekuwa siyo mkarimu. Ndipo mshukuru Mungu kwa uhusiano wako na familia na marafiki.

KUZAMA NDANI
Tumia rangi zinazong'aa kuchora picha ya nyumba kukiwa na jua na ndege nje na keki, zawadi na familia ndani. Halafu tumia rangi zisizong'aa kuchora nyumba ya pili kukiwa na mawingu na radi nje na ndugu wamekasirikiana ndani. Linganisha picha hizo. Zungumza kwa nini moja ina amani zaidi.

KWENDA NDANI ZAIDI
Familia zinaundwa na watu wenye haiba na hisia tofauti. Wakati mwingine wana familia wanajisikia furaha, na wakati mwingine wanajisikia kuchukia. Jinsi mtu anavyojisikia kusibadirishe nyumba yenye furaha kwa familia. Rumi 12:18 inasema, "Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.” Watu wote ni pamoja na wana familia wote. Kuendana na wote kwenye familia yako inaweza kuonekana kazi ngumu siku zingine. Lakini Mithali 17:1 inasema “Afadhali mego kavu pamoja na utulivu, Kuliko nyumba yenye karamu nyingi pamoja na magomvi.”
‭‭

MAJADILIANO
- Unatakiwa uweje kwa wana familia?
- Ufanyeje ili uwe mpatanishi kwenye familia wakati mtu amekasirika?
- Amani ya Mungu inawezaje kujaza nyumba yako, hata mnapokuwa na kutokukubaliana?

Andiko

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

God's Peace

Neno la Mungu linatuambia kwamba Hutoa amani " ipitayo ufahamu wote" (Wafilipi 4:7 SUV). Katika mafundisho haya ya siku nne, wewe na watoto wako muamgalie kwa makini maeneo katika maisha yetu tunapoweza kupata amani hiyo. Kila siku inajumuisha hitaji la maombi, kusoma maandiko kidogo na ufafanuzi, mazoezi ya kufanya, na maswali ya kujadili.

More

We would like to thank Focus on the Family for providing this plan. For more information, please visit: www.FocusontheFamily.com