Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Amani ya MunguMfano

God's Peace

SIKU 2 YA 4

AMANI KWA KUFUATA KANUNI ZA MUNGU

KUONGEA NA MUNGU
Mwambie Mungu unachopenda katika neno lake, Biblia. Mwambie kwa nini unapenda mstari au habari fulani, na mshukuru kwa ajili yake.

KUZAMIA
Nikiwa na mama na baba wakisimama karibu nami, jaribu kutembea kuzunguka chumba ukiwa umevaa viatu vya theluji, vya kuogelea au viatu ambavyo ni vikubwa. Unaweza kwenda umbali kiasi gani bila kujikwaa? Unadhani kanuni ya kutokuvaa viatu hivi ukiwa ndani itakuwa ni wazo jema? Elezea.

KWENDA NDANI ZAIDI
Tazama Zaburi 119:165: “Wana amani nyingi waipendao sheria yako, Wala hawana la kuwakwaza." Mungu anakuahidi msaada mkubwa wa amani unapofanya neno lake linavyosema. Kufuata kanuni za Mungu kunakusaidia kufanya makosa machache, na huna sababu ya kuwa na mashaka ya " kujikwaa" au kuumia kwa sababu ya maamuzi mabaya. Kuishi kulingana na neno la Mungu kunaruhusu amani yake kutawala moyo wako. Kweli! Kwa kumbukumbu neno la Mungu linasemaje, hakiki Zaburi 18:30, 19:8, 33:4.

MAJADILIANO
- Fikiria juu ya kanuni unayoifuata, kama kuvuka barabara kwenye punda milia au kutokukimbia kwenye ukumbi shuleni. Una uwezekano mkubwa wa kuumia unapofuata kanuni au usipozifuata? Elezea.
- Ni wakati gani umejisikia mwenye amani kwa sababu umelitii neno la Mungu?
- Unawezaje kurejesha amani ya Mungu baada ya kukosea?

Andiko

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

God's Peace

Neno la Mungu linatuambia kwamba Hutoa amani " ipitayo ufahamu wote" (Wafilipi 4:7 SUV). Katika mafundisho haya ya siku nne, wewe na watoto wako muamgalie kwa makini maeneo katika maisha yetu tunapoweza kupata amani hiyo. Kila siku inajumuisha hitaji la maombi, kusoma maandiko kidogo na ufafanuzi, mazoezi ya kufanya, na maswali ya kujadili.

More

We would like to thank Focus on the Family for providing this plan. For more information, please visit: www.FocusontheFamily.com