Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Amani ya MunguMfano

God's Peace

SIKU 1 YA 4

AMANI KATIKA USALAMA

KUONGEA NA MUNGU
Ni vitu gani vinakufanya uwe salama kila siku? Kuwa salama kunakupa kujisikia na amani. Mshukuru Mungu kwa mambo yanayokufanya uwe salama- mikanda ya usalama kwenye gari, vitasa vya milango, wazazi, polisi, wazima moto na hata viashiria vya moshi.

KUZAMIA
Nani au kitu gani kitapiga kelele utakapounguza mkate? ( wewe, mama yako au baba yako na taarifa ya moshi)

KWENDA NDANI ZAIDI
Katika siku za kale, watu walionywa juu ya moto kunapotokea moto. Watu waliokuwa wamelala wakati mwingine
hawasikii kelele za moto. Sasa hivi nyumba na majengo mengine yana viboksi vya plastiki vyenye betri vinavyotoa onyo kunapotokea moto. Unaweza kulala kwa amani bila shaka yoyote ya kutosikia kelele za moto mtaani. Mungu anakupa amani iliyo bora zaidi inayokusaidia kujisikia salama wakati wote. Yesu alisema katika Yohana 14:27 “Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.”
‭‭
KUJADILIANA
- Je, ni vitu gani unavyoogopa?
- Unapoogopa, unawezaje kukumbuka kuwa Mungu anataka kukupa amani yake.
- Unawezaje kufurahia zaidi amani ya Mungu leo?

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

God's Peace

Neno la Mungu linatuambia kwamba Hutoa amani " ipitayo ufahamu wote" (Wafilipi 4:7 SUV). Katika mafundisho haya ya siku nne, wewe na watoto wako muamgalie kwa makini maeneo katika maisha yetu tunapoweza kupata amani hiyo. Kila siku inajumuisha hitaji la maombi, kusoma maandiko kidogo na ufafanuzi, mazoezi ya kufanya, na maswali ya kujadili.

More

We would like to thank Focus on the Family for providing this plan. For more information, please visit: www.FocusontheFamily.com