Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

SIKU 29 YA 31

Nabii anatoa muhtasari wa ushindi wa Masihi jinsi utakavyokuwa katika ulimwengu huu. Mifano anayoitoa inalingana na hali ya kijiografia ya maeneo ya Palestina. Kwanza hali ya watu wa Mungu si nzuri. Adui zao wataanza kushangilia wakifikiri wamewashinda. Lakini angalia ni siku ya Bwana! Kwa ghafla ataleta ukombozi kwa watu wake kama alivyofanya kwenye bahari ya Shamu kwa wana wa Israeli. Ndivyo Kristo anavyoliponya Kanisa lake na kuwa Mfalme juu ya dunia yote. Tunaona hiyo tukilinganisha m. 9 na Ufu 17:14, Yuda naye atafanya vita juu ya Yerusalemu; na huo utajiri wa mataifa wa pande zote utakusanyika, dhahabu, na fedha, na mavazi; vitu vingi sana.... Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.

siku 28siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/