Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano
Ufunuo juu ya utukufu unaokuja wa Yerusalemu unaanza na habari ya hukumu ya Mungu juu ya maadui wa watu wake. Mara nyingi Mungu alipokuwa anawaadhibu Waisraeli alitumia mataifa ya kipagani, lakini sasa mkono wake ukiinuliwa kwa kuwatetea watu wake, hakuna adui awezaye kuwashambulia. Ingawa maadui wana nguvu na watu wa Mungu hawana, Yerusalemu utakaa mahali pake (m.6)! Hivyo itaonekana kuwa ndiye Mungu awapaye watu wake nguvu za kushinda, ili asiwepo mtu anayejivuna. Neno la Mungu linasema, Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi; kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana (1 Kor 1:27-31).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/