Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano
Mungu anamwita Zekaria kuchunga kondoo. Ni tendo la ishara kuonesha jinsi Bwana anavyochukizwa ingawa ni mchungaji mwema wa watu wake. Kwa hiyo Zekaria anavunja fimbo yake. Ni ishara ya kuwa agano la Bwana na watu wake limevunjika. Zekaria analipwa malipo ya mtumwa kwa huduma yake. "Ndivyo wanavyonilipa mimi," Bwana anasema (m.13), maana ni unabii wa jinsi Yesu alivyosalitiwa na kuondolewa. Katika Mt 27:9 tunasoma unabii ulivyotimizwa. Imeandikwa, Ndipo likatimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema, Wakavitwaa vipande thelathini vya fedha, kima chake aliyetiwa kima, ambaye baadhi ya Waisraeli walimtia kima. M.15-17 yaonesha kwamba tukimkataa Yesu kuwa mchungaji wetu, hakuna mwingine mwema: Kwa maana, tazama, mimi nitainua katika nchi hii mchungaji, ambaye hatawaangalia waliopotea, wala hatawatafuta waliotawanyika, wala hatamganga aliyevunjika, wala hatamlisha aliye mzima; bali atakula nyama ya wanono, na kuzirarua-rarua kwato zao. Ole wake mchungaji asiyefaa, aliachaye kundi! Upanga utakuwa juu ya mkono wake, na juu ya jicho lake la kuume; mkono wake utakuwa umekauka kabisa, na jicho lake la kuume litakuwa limepofuka.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/