Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

SIKU 24 YA 31

”Jiwe la pembeni”, ”msumari” na ”upinde wa vita” ni mifano inayomaanisha watawala wale ambao Bwana atawatokeza wawe mashujaa katika vita vyake vya kiroho. Watatoka "kwake" (m.4). Ukiangalia na m.3 unaona kwamba ni sawa na nyumba ya Yuda (m.3, Bwana wa majeshi ameliangalia kundi lake, yaani, nyumba ya Yuda, naye atawafanya kuwa kama farasi wake mzuri vitani). Habari hiyo inatuambia kuwa anayemfanya kila mmoja kuwa kama alivyo, ndiye Bwana. Tafakari tena Mungu anavyosema katika m.6, Nami nitaitia nguvu nyumba ya Yuda, nami nitaiokoa nyumba ya Yusufu, nami nitawarudisha, kwa maana nawaonea rehema; nao watakuwa kana kwamba sikuwatupa; kwa maana mimi ni Bwana, Mungu wao, nami nitawasikia! Somo latabiri jinsi Mungu atakavyokomboa na kukusanya watu wake wote katika nchi yake. Yuda anawakilisha makabila 2 ya kusini na Yusufu makabila 10 ya kaskazini. Mungu mwenyewe ataondoa upinzani wote.

siku 23siku 25

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022

Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/