Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022Mfano
Nimejipindia Yuda, nimeujaza upinde wangu Efraimu; nami nitawaondokesha wana wako, Ee Sayuni, wapigane na wana wako, Ee Uyunani, nami nitakufanya wewe kuwa kama upanga wa shujaa. Pamoja na habari hii katika m.13 mistari miwili ya kwanza ya somo la leo yatuambia kuwa ufalme wa amani hautaletwa bila upinzani, lakini hatimaye utakuwepo. Ni kwa sababu Mungu ataonekana juu ya watu wake kama Bwana wa majeshi, akiwapigania na kuwalinda. Na Bwana, Mungu wao, atawaokoa siku hiyo, Kama kundi la watu wake; Kwa maana watakuwa kama vito vya taji, Vikimeta-meta juu ya nchi yake. Maana wema wake, jinsi ulivyo mwingi! Na uzuri wake, jinsi ulivyo mwingi! Nafaka itawasitawisha vijana wanaume, Na divai mpya vijana wanawake (m.16-17). Katika mistari hii twaona tokeo lake, Mungu akiwapigania watu wake. Siku moja ufalme wenye ushindi, amani, wema, uzuri na ustawi upo! Sababu ni Bwana mwenyewe. Atawaokoa na kuwaongoza watu wake kama mchungaji mwema anavyofanya kwa kundi lake la kondoo (m.16a, Bwana, Mungu wao, atawaokoa siku hiyo, kama kundi la watu wake). Jinsi wema wake ulivyo mwingi!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Agosti pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Zakaria. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/