Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano
Mtunzi wa zaburi hii anaendelea kuelezea heshima na utukufu wa mfalme huyu akihusianisha na fahari na mapambo ya sherehe ya arusi. Kisha anatoa angalizo kwa malkia mpya (bibi arusi), abadilishe tabia yake na kuwa mwaminifu kwa mumewe. Picha hii inahusu Yesu na Kanisa. Hivyo kanisa, yaani mimi na wewe tulioposwa na Yesu Kristo tunapaswa tubadilishe tabia zetu na kuwa waaminifu wa Yesu. Yeye ndiye Bwana Arusi. Katika m.10-12 imeandikwa kwamba mfalme atautamani uzuri wako, maana ndiye bwana wako, nawe umsujudie. Hulingana na ilivyoandikwa katika Ufu 19:6-8 kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari. Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi. Tumngojee Bwana Yesu. Anakaribia!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/