Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano
Dunia ya leo ina tabaka la maskini na matajiri. Wanyonge na wenye nguvu. Matajiri na wenye uwezo hawawakumbuki wanyonge na badala yake wanawanyonya, wanaendelea kijilimbikizia mali bila kuwakumbuka maskini. Zaburi hii inawaasa wenye navyo kuwasaidia wasio navyo na kuwatunza, kwani Mungu atawapa thawabu: Heri amkumbukaye mnyonge; Bwana atamwokoa siku ya taabu. Bwana atamlinda na kumhifadhi hai, naye atafanikiwa katika nchi; ... Bwana atamtegemeza alipo mgonjwa kitandani (m.1-3). Swali la kuijiuliza leo ni hili ni mara ngapi tunawajali maskini na wanyonge? Daudi katika Zaburi hii anasema: Heri amkumbukaye mnyonge; Bwana atamwokoa siku ya taabu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/