Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano
Kuna wakati watu wa Mungu wanapata shida pamoja na kwamba wanaendelea kumpenda na kumheshimu Mungu wao. Tena, wakati mwingine Mungu mwenyewe anaruhusu mateso yatokee kama ilivyokuwa kwa Ayubu. Ni wazi mateso yake yalikuwa na kibali cha Mungu (Ayu 1:12, Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe). Mtunzi wa zaburi hii anamlilia Mungu kuwa mbona amemwacha. Pia Mungu ameruhusu maadui zake wamwaibishe na kumfanya mtumwa wao. Mwandishi haoni sababu ya mateso hayo. Lakini wakati huohuo anakumbuka kuwa Mungu yu pamoja naye. Hiyo ni sababu ya ombi lake katika m.26, Uondoke, uwe msaada wetu, utukomboe kwa ajili ya fadhili zako. Vivyo hivyo katika taabu zetu, Mungu yu pamoja nasi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/