Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano
Siku hizi, tunasikia misukosuko mingi na inatishia usalama. Mwandishi wa zaburi hii anatukumbusha kuwa mambo hayo yalikuwepo tangu huko nyuma. Anaonyesha kuwa Mungu alianza kuwapigania watu wake tangu mwanzo kabisa wakiwa utumwani Misri. Aliwabariki wazee wetu kwani walikuwa ni uzao wa Ibrahimu ambaye Yeye aliahidi kumbariki. Kwa hiyo tunapoona ulimwengu mzima ukiwa unatikiswa na vurugu nyingi bado tuna imani kwamba huyo Mungu aliyewapigania wazee wetu anaweza kutusaidia hata sisi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Ufunuo na masomo maalumu kwa ajili ya Sikukuu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/