BibleProject | Tafakari ya Ujio wa YesuMfano
Yesu anafundisha wafuasi wake akisema, "watu wanapowakana au kuwatesa kwa kunifuata, shangilia, furahia, kwa sababu thawabu yenu ni kubwa mbinguni." Tunaona katika mafundisho ya Yesu kwamba furaha ya kweli inaweza kustahimili changamoto zozote kwasababu msingi wake sio hali iliyopo sasa. Badala yake inamtegemea Mungu na ahadi zake za mustakabali wa milele wa watu wake.
Soma:
Mathayo 5:11-12, Matendo 13:50-52, Waebrania 12:1-3
Tafakari:
Kwa mujibu wa vifungu hivi, furaha inaweza kudumishwa vipi hata katika hali za huzuni na kutisha?
Tumia muda kuchambua Waebrania 12:1-3. Yesu alivumilia maumivu makubwa kwa sababu aliweza kuona furaha kubwa inayozidi mateso yake. Katika kifungu hiki, wafuasi wa Yesu wanaitwa kuvumilia ugumu huku wakimwangazia Yesu; anakuwa furaha iliyowekwa mbele yao. Unafiriki "kuangaza macho yako kwa Yesu" kunamaanisha nini kihalisia?
Geuza tafakuri zako kuwa sala kutoka moyoni mwako kwenda kwa Mungu.
Kuhusu Mpango huu
BibleProject ilibuni Tafakari ya Ujio wa Yesu ili kuhamasisha watu mmoja mmoja, vikundi vidogo vidogo, na familia kusherehekea majilio, au kuwasili kwa Yesu. Mwongozo huu wa wiki nne unashirikisha video za kikatuni, mihutasari mifupi, na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia washiriki kuchunguza maana ya Biblia ya tumaini, amani, furaha, na upendo. Chagua mwongozo huu ili kujifunza jinsi maadili haya manne yamefika ulimwenguni kupitia kwa Yesu.
More
Tungependa kushukuru BibleProject kwa kutoa Mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://bibleproject.com