BibleProject | Tafakari ya Ujio wa YesuMfano
Yesu alipoulizwa kuhusu amri muhimu zaidi katika Agano la Kale katika Biblia ya Kiebrania, anajibu kwa kunukuu kutoka kwa sala ya kale inalojulikana kama Shema, “mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote.” Lakini siyo hilo tu. Yesu anaendelea kwa upesi na kusema kwamba amri nyingine kutoka katika Biblia ya Kiebrania ni muhimu zaidi pia, “mpende jirani yako kama unavyojipenda." Kwa hivyo ni ipi iliyo muhimu zaidi? Kwa Yesu, zote mbili ni muhimu kwa sababu amri ya kwanza haiwezi kutiiwa bila kutii ya pili. Haziwezi kutenganishwa. Upendo wa mtu kwa Mungu huonyeshwa na upendo wake kwa wengine.
Soma:
Marko 12:29-31, Kumbukumbu la Torati 6:5, Mambo ya Walawi 19:18
Tafakari:
Kuwa makini kuhusu Yesu anachosema baada ya kunukuu kutoka katika Biblia ya Kiebrania. Ni maswali gani, mawazo, au hisia zinaibuka unavyofikiri kuhusu maneno yake? Chambua vifungu kutoka katika Kumbukumbu la Torati na Mambo ya Walawi. Unaona nini? Hili linakuathiri vipi leo?
Geuza tafakuri zako kuwa sala kwa Mungu kutoka moyoni mwako.
Kuhusu Mpango huu
BibleProject ilibuni Tafakari ya Ujio wa Yesu ili kuhamasisha watu mmoja mmoja, vikundi vidogo vidogo, na familia kusherehekea majilio, au kuwasili kwa Yesu. Mwongozo huu wa wiki nne unashirikisha video za kikatuni, mihutasari mifupi, na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia washiriki kuchunguza maana ya Biblia ya tumaini, amani, furaha, na upendo. Chagua mwongozo huu ili kujifunza jinsi maadili haya manne yamefika ulimwenguni kupitia kwa Yesu.
More
Tungependa kushukuru BibleProject kwa kutoa Mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://bibleproject.com