Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Tafakari ya Ujio wa YesuMfano

 BibleProject | Tafakari ya Ujio wa Yesu

SIKU 17 YA 28

Njia za Mungu hutoa furaha halisi na hekima kwa wanadamu (tazama Zaburi 19:7-8). Lakini Shetani anakusudia kuwapotosha wanadamu kuona njia zao kama ndio zilizojawa na hekima (tazama Mwanzo 3:6). Ni rahisi kupotoshwa kwa sababu udanganyifu wa Shetani mara nyingi hutupatia starehe ya muda mfupi. Lakini wanadamu wanapochagua maagizo yao wenyewe badala ya maagizo ya Mungu, hawatoweza kupata furaha ya kweli na ya kudumu wanayotafuta.

Soma:

 Zaburi 19:7-11, Mwanzo 3:1-7 

Tafakari: 

Linganisha na kutofautisha vifungu hivi viwili vya siku. Ni maneno na dhana gani zinazorudiwa katika vifungu vyote viwili? Unatambua nini? Omba upate imani mpya juu ya nia njema za Mungu kwako. Mwambie ukweli kuhusu maeneo uliyopingana naye au kuwa na wasiwasi naye na uombe unachohitaji ili kufuata uongozi wake leo. 



siku 16siku 18

Kuhusu Mpango huu

 BibleProject | Tafakari ya Ujio wa Yesu

BibleProject ilibuni Tafakari ya Ujio wa Yesu ili kuhamasisha watu mmoja mmoja, vikundi vidogo vidogo, na familia kusherehekea majilio, au kuwasili kwa Yesu. Mwongozo huu wa wiki nne unashirikisha video za kikatuni, mihutasari mifupi, na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia washiriki kuchunguza maana ya Biblia ya tumaini, amani, furaha, na upendo. Chagua mwongozo huu ili kujifunza jinsi maadili haya manne yamefika ulimwenguni kupitia kwa Yesu.

More

Tungependa kushukuru BibleProject kwa kutoa Mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://bibleproject.com