Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kuwa Karibu Na Mungu Kila SikuMfano

 Kuwa Karibu Na Mungu Kila Siku

SIKU 6 YA 14

Omba Kuhusu Kila Kitu na Usiogope Chochote

Iweni hodari, mpige moyo konde, ninyi nyote mnaomngoja Bwana! - ZABURI 31:24

Wakati mwingine uliopita, nilihisi Bwana akinenea maneno haya: “Omba kuhusu kila kitu na usiogope chochote.” Kwa muda wa wiki kadhaa zilizofuatia, alinionyesha vitu tofauti kuhusu maombi dhidi ya hofu. Wingi wa vitu hivyo vilikabiliana na maeneo madogo ambamo hofu ingejaribu kuingia katika maisha yangu na kunisababishia shida. Akanionyesha kwamba katika kila jambo, bila kujali ukubwa au umuhimu wake au udogo au kutokuwa kwalo na umuhimu, suluhu ilikuwa kuomba. 

Wakati mwingine tunakuwa waoga kwa sababu ya kufikiria hali zetu. Kadri tunavyoifikiria shida yetu, ndivyo tunavyokuwa waoga zaidi. Badala yake tunaweza kuchagua kuweka mawazo yetu juu ya Mungu. Ana uwezo wa kushughulikia chochote ambacho huenda kikatukumba katika maisha. 

Mungu ameahidi kututia nguvu, kutufanya sugu kwa matatizo, kutusaidia na kutushika kwa mkono wa kuume wa haki yake (Isaya 41:10). Anatuamuru pia kutoogopa. Lakini kumbuka, hatuamrishi kutohisi woga, lakini badala yake kutoruhusu itudhibiti.  

Bwana anatuambia leo, “Msiogope, nitawasaidia.” Lakini huwa hatushuhudii usaidizi wa Mungu hadi tusalimishe kila kitu na kuwa watiifu ya kutosha kuchukua hatua ya imani. 

Usikate tamaa unapohisi woga. Mwamini Bwana na uendelee kusonga mbele.

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

 Kuwa Karibu Na Mungu Kila Siku

Katika mpango huu wa ibada ya Siku 14 Joyce husaidia wasomaji kufikia maisha ya ujasiri zaidi, yenye furaha kwa kukua karibu katika uhusiano wao na Mungu.

More

Tungependa kuwashukuru Mawaziri wa Joyce Meyer kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tv.joycemeyer.org/kiswahili/