Kuwa Karibu Na Mungu Kila SikuMfano
Amani katika Hali Yoyote
Huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. - 1 PETRO 5:7
Amani ipitayo ufahamu wote ni kitu kikuu cha kufurahia (Wafilipi 4:7). Wakati ambao kulingana na hali, unafaa kufadhaika, kushtuka, kuchanganyikiwa na kuwa na wasiwasi, unapata kwamba una amani, hilo halielezeki. Ulimwengu una njaa ya aina hii ya amani. Huwezi kuinunua; haiuzwi. Ni kipawa cha bure kutoka kwa Mungu ambacho huja kutokana kukaa kwa ukaribu wa ndani naye, na matokeo yake ni furaha isiyosemeka.
Amani huja unapompa Bwana mzigo wako—unapochagua kumtwika fadhaa zako badala ya kujitwika mwenyewe. Itakuwa bora ukifanya hivyo haraka iwezekanavyo. Mtwike Mungu shida yako mara tu moja inapotokea. Hata usijaribu kuzishughulikia mwenyewe. Kadri unavyongoja kwa muda mrefu, ndivyo inavyokuwa vigumu kuwa huru kutokana na wasiwasi na fadhaa.
Kwa sababu Mungu ameahidi kwamba yuko nasi kila wakati, tunaweza kuwa na amani na furaha ya ajabu… hata katikati ya dhiki. Ni yeye peke anayeweza kutupatia hayo. Hiyo ndiyo maana ya kuwa na amani inayopita ufahamu wote.
Aaminiye aliye na amani ya Mungu kupitia kwa uhusiano wake na Yesu anaweza kuwa na amani katikati mwa dhoruba mbaya kabisa ya maisha.
Kuhusu Mpango huu
Katika mpango huu wa ibada ya Siku 14 Joyce husaidia wasomaji kufikia maisha ya ujasiri zaidi, yenye furaha kwa kukua karibu katika uhusiano wao na Mungu.
More
Tungependa kuwashukuru Mawaziri wa Joyce Meyer kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tv.joycemeyer.org/kiswahili/