Kuwa Karibu Na Mungu Kila SikuMfano
Nguvu za Tumaini
Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, ndivyo utakavyokuwa uzao wako. Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwishapata umri wa miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara. Lakini akiiona ahadi ya Mungu, hakusita kwa kutokuamini bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu. - WARUMI 4:18–20
Katika huduma yetu tunataka kusaidia watu zaidi kila mwaka, na tunaamini Mungu anataka tukue. Lakini tunatambua pia kuwa, iwapo Mungu ana mpango tofauti, na tuhitimishe mwaka wetu bila makuzi, hatuwezi kuacha hali hiyo idhibiti furaha yetu.
Tunaamini kwa sababu ya vitu vingi, lakini zaidi ya yote, tunamwamini Mtu fulani. Huyo Mtu ni Yesu. Huwa hatujui wakati wote litakalofanyika. Tunajua tu kuwa litafanyika ili tukapate wema!
Imeripotiwa kuwa Ibrahimu, baada ya kupima hali yake, (hakupuuza hali iliyokuwa), alifikiri kuhusu udhaifu wa mwili wake na utasa wa tumbo la uzazi la Sarai. Ingawa matumaini yote ya urazini wa mwanadamu hayakuwa, alitumainia kwa imani. Ibrahimu alikuwa na fikra chanya kuhusu hali hasi kabisa!
Waebrania 6:19 inatuambia kuwa, tumaini ni nanga ya moyo. Tumaini ndiyo nguvu inayotuimarisha wakati wa majaribu. Usiache kuwa na tumaini. Usiogope kutumaini. Hakuna anayeweza kuahidi kwamba hutawahi kusikitika. Lakini unaweza kuwa na tumaini kila mara na kuwa na fikra chanya.
Kuwa na tarajio la matumaini tele kila siku ya maisha yako.
Kwa ujumbe zaidi kama huu kutoka kwa Joyce tafadhali tembelea: https://tv.joycemeyer.org/kiswahili/
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Katika mpango huu wa ibada ya Siku 14 Joyce husaidia wasomaji kufikia maisha ya ujasiri zaidi, yenye furaha kwa kukua karibu katika uhusiano wao na Mungu.
More
Tungependa kuwashukuru Mawaziri wa Joyce Meyer kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tv.joycemeyer.org/kiswahili/