Kuwa Karibu Na Mungu Kila SikuMfano
Yesu ni Mwamba Wako
Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi. - 2 WAKORINTHO 1:20
Mahali kwingi katika Biblia kwa mfano, 1 Wakorintho 10:4, Yesu anarejelewa kama Mwamba. Mtume Paulo anaendelea kutuambia katika Wakolosai 2:7 kwamba, tuwe wenye shina na wenye kujengwa katika Yesu.
Tukiacha mizizi yetu ifungike kwa kumzunguka Yesu, tutakuwa katika hali nzuri. Lakini ikifungika kwa kuzunguka kitu au mtu mwingine, tuko mashakani.
Hakuna mtu au kitu ambacho kinaweza kuwa na uthabiti na cha kutegemewa kama Yesu. Ndiyo kwa sababu ni muhimu kuelekeza watu kwa Yesu. Wanadamu wanaweza kushindwa wakati wowote. Lakini Yesu hawezi kushindwa. Tia tumaini lako lote bila kubadilika ndani yake. Sio ndani ya mwanadamu, sio ndani ya hali, sio ndani ya kitu chochote.
Ukikosa kutia imani na tumaini lako katika mwamba wa wokovu wako, unaelekea kwenye masikitiko ambayo husababisha mtamauko na uharibifu. Tunafaa kuwa na hakikisho kuu katika upendo wa Mungu juu yetu kiasi kwamba hata kitu gani kije kinyume nasi, tunajua ndani mioyoni mwetu kwamba yuko nasi na hatatuacha tuaibike.
Sisi ni waflisi katika uwezo wetu wenyewe kando na Yesu. Bila Mungu, hatuwezi, tukiwa naye, hakuna kitakachokuwa kigumu kwetu.
Kuhusu Mpango huu
Katika mpango huu wa ibada ya Siku 14 Joyce husaidia wasomaji kufikia maisha ya ujasiri zaidi, yenye furaha kwa kukua karibu katika uhusiano wao na Mungu.
More
Tungependa kuwashukuru Mawaziri wa Joyce Meyer kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tv.joycemeyer.org/kiswahili/