Soma Biblia Kila Siku 11/2020Mfano
Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu(m.2). "Maziwa ... yasiyoghoshiwa"lina maana ya maziwa yasiyochanganywa, maziwa safi. "Maziwa ya akili", tafsiri nzuri zaidi ni "maziwa ya neno". Mtoto mchanga huhitaji maziwa ili akue vizuri! Ukimpa maziwa yasiyo safi au pombe, mwili wake utadhoofika. Vilevile Mkristo asitamani tena mambo yasiyo safi ambayo amekombolewa nayo (m.1: Wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote). Bali alitamani nenoili kwa hilo akue katika imani!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 11/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz