Soma Biblia Kila Siku 05/2020Mfano
Mwanadamu hapendi kuyaweka wazi mambo yake. Kinyume chake huwa anatoroka na kufichama (ling. Mwa 3:10, Adamu akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha). Mazoea haya yanatofautiana na hali aliyokuwa nayo mtumishi wa Mungu Ayubu. Wakosoaji wake walimwona ni mdhambi. Lakini badala ya kujifungia ili kuepuka mashtaka yao, Ayubu anafunguka. Anajipambanua. Anajiweka dhahiri mbele ya Mungu (m.35,Laiti ningekuwa na mtu wa kunisikia! (Tazama, sahihi yangu ni hii, Mwenyezi na anijibu). Makosa hufichwa kwa uongo, lakini afichaye dhambi zake hatafanikiwa (Mit 28:13). Unaweza kuwatoroka watu, siyo Mungu. Unajifunza jambo gani hapa?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Ayubu, Zaburi na 1 Yohana. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz