Ayu 31:33-40
Ayu 31:33-40 SUV
Ikiwa kama mwanadamu nimeyafunika makosa yangu, Kwa kuuficha uovu wangu kifuani mwangu; Kwa sababu niliwaogopa mkutano mkubwa, Na dharau la jamaa lilinitia hofu, Hata nilinyamaa kimya, nisitoke mlangoni- Laiti ningekuwa na mtu wa kunisikia! (Tazama, sahihi yangu ni hii, Mwenyezi na anijibu); Laiti ningekuwa na hayo mashitaka yaliyoandikwa na adui yangu! Hakika ningeyachukua mabegani; Ningejifungia mfano wa kilemba. Ningemwambia hesabu ya hatua zangu Ningemkaribia kama vile mkuu. Kama nchi yangu yalia juu yangu, Na matuta yake hulia pamoja; Kama nimeyala matunda yake pasipo kulipa, Au kama nimewafanya wenyewe kupotewa na uhai; Miiba na imee badala ya ngano, Na magugu badala ya shayiri. Maneno ya Ayubu yamekoma hapa.