Yobu 31:33-40
Yobu 31:33-40 Biblia Habari Njema (BHN)
Je nimeficha makosa yangu kama wengine? Je nimekataa kukiri dhambi zangu? Sijaogopa kusimama mbele ya umati wa watu, wala kukaa kimya au kujifungia ndani, eti kwa kuogopa kutishwa na dharau zao. Laiti angekuwapo mtu wa kunisikiliza! Naweza kutia sahihi yangu katika kila nilichosema. Namwambia Mungu Mwenye Nguvu anijibu! Laiti mashtaka wanayonitolea maadui zangu yangeandikwa! Ningeyavaa kwa maringo mabegani na kujivisha kichwani kama taji. Ningemhesabia Mungu kila kitu nilichofanya, ningemwendea kama mwana wa mfalme. Kama nimeiiba ardhi ninayoilima, nikasababisha mifereji yake iomboleze, kwa kufaidika na mazao yake bila kulipa na kusababisha kifo cha wenyewe, basi miiba na iote humo badala ya ngano, na magugu badala ya shayiri.” Mwisho wa hoja za Yobu.
Yobu 31:33-40 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ikiwa kama mwanadamu nimeyafunika makosa yangu, Kwa kuuficha uovu wangu kifuani mwangu; Kwa sababu niliwaogopa mkutano mkubwa, Na dharau la jamaa lilinitia hofu, Hata nilinyamaa kimya, nisitoke mlangoni. Laiti ningekuwa na mtu wa kunisikia! (Tazama, sahihi yangu ni hii, Mwenyezi na anijibu); Laiti ningekuwa na hayo mashitaka yaliyoandikwa na adui yangu! Hakika ningeyachukua mabegani; Ningejifunga mfano wa kilemba. Ningemwambia hesabu ya hatua zangu Ningemkaribia kama vile mkuu. Kama nchi yangu imelia juu yangu, Na matuta yake hulia pamoja; Kama nimeyala matunda yake pasipo kulipa, Au kama nimewafanya wenyewe kupotewa na uhai; Miiba na imee badala ya ngano, Na magugu badala ya shayiri. Maneno ya Ayubu yamekoma hapa.
Yobu 31:33-40 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ikiwa kama mwanadamu nimeyafunika makosa yangu, Kwa kuuficha uovu wangu kifuani mwangu; Kwa sababu niliwaogopa mkutano mkubwa, Na dharau la jamaa lilinitia hofu, Hata nilinyamaa kimya, nisitoke mlangoni- Laiti ningekuwa na mtu wa kunisikia! (Tazama, sahihi yangu ni hii, Mwenyezi na anijibu); Laiti ningekuwa na hayo mashitaka yaliyoandikwa na adui yangu! Hakika ningeyachukua mabegani; Ningejifungia mfano wa kilemba. Ningemwambia hesabu ya hatua zangu Ningemkaribia kama vile mkuu. Kama nchi yangu yalia juu yangu, Na matuta yake hulia pamoja; Kama nimeyala matunda yake pasipo kulipa, Au kama nimewafanya wenyewe kupotewa na uhai; Miiba na imee badala ya ngano, Na magugu badala ya shayiri. Maneno ya Ayubu yamekoma hapa.
Yobu 31:33-40 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
kama nimeifunika dhambi yangu kama wanadamu wengine wafanyavyo, kwa kuficha hatia yangu moyoni mwangu, kwa sababu ya kuogopa umati wa watu, na hivyo kuwa na hofu ya kudharauliwa na jamaa, nikanyamaza kimya nisitoke nje ya mlango: (“Laiti kama angekuwepo mtu wa kunisikia! Tazama sasa ninatia sahihi kwenye utetezi wangu: Mwenyezi na anijibu; mshtaki wangu na aweke mashtaka yake kwenye maandishi. Hakika ningeyavaa begani mwangu, ningeyavaa kama taji. Ningempa hesabu ya kila hatua yangu, ningemwendea kama mwana wa mfalme.) “Kama nchi yangu inalia dhidi yangu, na mifereji yake yote imelowana kwa machozi, kama nimekula mazao yake bila malipo, au kuvunja mioyo ya wapangaji wake, basi miiba na iote badala ya ngano, na magugu badala ya shayiri.” Mwisho wa maneno ya Ayubu.