Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayubu 31:33-40

Ayubu 31:33-40 NEN

kama nimeifunika dhambi yangu kama wanadamu wengine wafanyavyo, kwa kuficha hatia yangu moyoni mwangu, kwa sababu ya kuogopa umati wa watu, na hivyo kuwa na hofu ya kudharauliwa na jamaa, nikanyamaza kimya nisitoke nje ya mlango: (“Laiti kama angekuwepo mtu wa kunisikia! Tazama sasa ninatia sahihi kwenye utetezi wangu: Mwenyezi na anijibu; mshtaki wangu na aweke mashtaka yake kwenye maandishi. Hakika ningeyavaa begani mwangu, ningeyavaa kama taji. Ningempa hesabu ya kila hatua yangu, ningemwendea kama mwana wa mfalme.) “Kama nchi yangu inalia dhidi yangu, na mifereji yake yote imelowana kwa machozi, kama nimekula mazao yake bila malipo, au kuvunja mioyo ya wapangaji wake, basi miiba na iote badala ya ngano, na magugu badala ya shayiri.” Mwisho wa maneno ya Ayubu.