Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 03/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

SIKU 8 YA 31

Wakamletea Daudi kichwa cha Ishboshethi huko Hebroni (m.8). Waliamini Daudi atafurahi kwa habari ya kifo cha adui yake, lakini sivyo. Badala yake alikasirika na kuagiza hao wauawe. Kwa nini alifanya hivi? Ni kwa sababu Daudi ni mcha Mungu moyoni mwake. Hawezi kumwua kiongozi aliyewekwa na Mungu mwenyewe. Sauli alikuwa ametawazwa na Mungu, na Daudi hakutaka kamwe kupata mamlaka kwa njia isiyo halali! Astahiliye heshima apewe heshima! Zingatia maneno yafuatayo ya Biblia: Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu. … Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima(Rum 13:1-2 na 7).Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme(1 Pet 2:17). 

siku 7siku 9

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2020

Soma Biblia Kila Siku 03/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Samweli, Mathayo na Zaburi. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kusoma na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz