Maombi HatariMfano
Nisumbue
Tunachokiomba ni muhimu. Lakini siyo tuu ni muhimu, bali pia hufunua.
Yaliyomo kwenye maombi yetu yanatuonesha zaidi jinsi tulivyo na uhusiano wetu na Mungu kuliko watu wengi wanavyoweza kufikiria. Tunachoomba kinaonesha kile tunachokiamini kuhusu Mungu. Kama maombi yetu mengi ni "kwa ajili yetu" au " yale yanayoonekana ya muhimu kwetu", ndipo yaliyomo kwenye maombi yetu yanaashiria kwamba tunaamini, ndani yetu, kwamba Mungu anaishi kimsingi kwa ajili yetu.
Kwa hiyo jitizame na ufanye ukaguzi wa maombi. Fikiria juu ya kila kitu ulichoomba siku za karibuni--siyo maisha yako yote, siku saba tuu zilizopita. Unaweza kuandika kwenye daftari au kuchapa kwenye simu yako na kuorodhesha vitu vyote tofauti ulivyovitaja mbele za Mungu juma lililopita. Hebu tafakari kwa muda. Unakumbuka? Uliombea nini? Ulimuomba Mungu afanye nini?
Sasa jibu waziwazi. Kama Mungu angesema ndiyo kwa kila ombi ulilofanya kwa siku saba zilizopita, ulimwengu ungekuwaje tofauti?
Kama maombi yako yalikuwa ya kawaida, ya usalama, ndipo yawezekana ungekuwa na siku njema, kufika salama, au kufurahia baraka tele, vyakula na cocacola.
Kwa miaka mingi, kama ningefanya ukaguzi wa maombi, matokeo yangekuwa madogo. Kama Mungu angefanya kila kitu kwa juma zima nililomuomba kufanya, ulimwengu ungekuwa hauna tofauti hata kidogo. Kusema ukweli, majuma mengine nisingeomba chochote. Majuma mengine, yawezekana niliomba, lakini maombi yalikuwa juu yangu tuu, na hayo hayabadili sana jumla ya mambo.
Maombi yangu yalikuwa salama sana.
Nilikuwa na fursa kwa muumba na mshikilia anga. Mimi ndiye. Alfa na Omega. Mwanzo na Mwisho. Mwenye nguvu zote, aliyepo, ajuaye yote na kuweza kutuma moto kutoka mbinguni, kufunga makanwa ya simba wenye njaa, au kutuliza dhoruba. Na nilichomuomba kufanya ilikuwa nilinde na nisaidie niwe na siku njema.
Kwa miaka mingi, sikutaka kuingiliwa. Lakini baada ya kuomba maombi ya hatari zaidi, nikagundua kwamba ule upole wa Mungu wa kusemesha kungeniingilia mara kwa mara mipango yangu binafsi na angenielekeza kwenye mapenzi yake ya milele.
Imani yangu ni imara.
Maisha yangu ni tajiri.
Moyo wangu umejaa.
Fikiria kungekuwa na tofauti gani kama ungeomba kwa uwazi zaidi. Kama ulijihatarisa zaidi. Kama ungekuwa muwazi kwa kile Mungu angefanya ndaniyako badala ya kutumaini tuu kwamba atafanya kitu kwa ajili yako. Ingekuwaje kama ungeomba maombi ya ujasiri? Kuota ndoto kubwa? Kwa bidii kumtafuta Yesu kwa kuthubutu, kwa imani ya kujikana?
Ni muda wa kubadili jinsi unavyoomba. Ni muda wa kuacha maombi salama, starehe, yakujirudia, na maombi ya urahisi. Ni wakati wa kuomba kwa ujasiri, kujihatarisha, kujifunua katika njia mbali mbali kuelekea mwisho bora. Ni wakati wa kuanza kuomba maombi ya hatari. Ni wakati wa kusumbuliwa.
Kama kweli unataka kuleta tofauti duniani, unahitaji nguvu kutoka mbinguni. Kama unataka maisha yako yawe na maana, ni wakati wa kuomba sana, kwa ujasiri, na maombi ya kuthubutu.
Mtafute Mungu na ota ndoto kubwa. Kataa kusikia kushindwa. Ni wakati wa kutoka. Kuamini. Kuthubutu. Kuamini. Maisha yako siku zote hutajisikia salama. Na itachukua imani. Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu.
Unangoja nini?
Jifunza zaidi kuhusu kitabu kipya cha Craig Groeschel’s, kuhusuDangerous Prayers.
Kuhusu Mpango huu
Umechoka kujali usalama katika imani yako? Uko tayari kukabili hofu zako, kujenga imani yako, na kufikia uwezo wako kamili? Mpango huu wa Biblia wa siku 7 kutoka kwenye kitabu cha Mchungaji Craig Groeschel wa Life.Church, "Dangerous Prayers" yaani Maombi Hatari, unakujasiri uombe bila kujali usalama—kwa sababu kumfuata Yesu haukufaa kuwa salama salmini.
More