Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maombi HatariMfano

Dangerous Prayers

SIKU 6 YA 7

Nitume mimi

Kama mchungaji kwa miongo kadha, nimeona mwenyewe maombi ya ndani sana ya maelfu ya watu. Kila juma, maelfu ya mahitaji ya watu yanakuja kanisani kwetu, kutokana na kadi za maombi yatokanayo na ibada zetu au kwa njia ya simu wakati wa ibada zetu au mitandao ya kijamii au app ya kanisa. Kwa hiyo hutashangaa kuona maneno yanayojirudia nayosikia kila juma na ndiyo napenda kutimiza: " Mchungaji, unaweza kuniombea.......”

Ninahesabu kwamba ni fursa, heshima, na wajibu mzuri kusimama na kuinua mahitaji mbele za kiti cha enzi cha Mungu, nikimuomba rehema, kutembea, kuongoza, kukutana na mahitaji, kutenda, kufanya miujiza kwa watu ninaowajua na kuwapenda. Kila juma mtu anaomba kwamba Mungu amponye mpendwa wake na saratani, amsaidie jirani apate kazi, au kurejesha ndoa yenye matatizo. Wanafunzi wanaleta maombi ili wajiunge na chuo wanachokitaka, kusaidia kulipia chuo, au kushughulika na maumivu ya kuachana kwa wazazi wao. Wengine wanaombea wenzi wao. Wengine wanaombea msaada wa kuwasamehe waliowaumiza. 

Ijapokuwa maombi yanatofautiana, watu wanamuomba Mungu kufanya jambo kwa ajili yao au mtu wanayempenda. Mungu, nisaidie. Mungu, msaidie mtu ninayempenda. Bwana, ninakuhitaji....Baba, tafadhali.....? 

Mungu, fanya jambo kwa ajiliyangu

Tafadhali nisikilize...tunatakiwa kuomba namna hii. Siku zote tunatakiwa tuujue uwepo wa Mungu, nguvu za Mungu, amani ya Mungu kuingilia maishani mwetu. Tunatakiwa tumuombe Mungu atende miujiza kwa niaba yetu. Tunatakiwa kuwainua wapendwa wetu na kujikumbusha jinsi Mungu anavyoweza kutembea katika maisha yao. Tunatakiwa kumtafuta Bwana kwa mahitaji yetu yote.

Lakini hatutakiwi kuishia hapo.

Itakuwaje kama badala ya kumwomba Mungu kufanya jambo kwa ajili yetu, tukaomba maombi ya hatari, ya kujikana na kujitoa kwa Baba yetu wa mbinguni?

Itakuwaje kama tukaomba labda maoni ya hatari sana?

“Nitume mimi, Bwana. Nitumie.”

Isaya aliomba maombi ya kujitoa kikamilifu mbele za Mungu. Nabii wa Agano la Kale anaelezea kukutana kwake na Mtakatifu wakati Mungu alipouliza " Nimtume nani? Na ni nani atakwenda kwa niaba yetu"? (Isa. 6:8a) Na pasipokujua kwa undani, pasipokujua wapi na lini, Isaya aliomba maombi haya, maombi ya kubadirisha: “Niko hapa. Nitume mimi!!” (Isa. 6:8b).

Kumbuka kwamba Isaya hakuuliza maelezo yoyote. Hakumuuliza Mungu niende wapi. Au niende lini. Au kutatokea nini. Ndiyo maana maombi haya yanaonekana ni hatari sana. " Mungu, nitume mimi. Nitumie. Siulizi taarifa zaidi. Sihitaji kujua faida. Au kama itakuwa rahisi. Au kama nitafurahia. Kwa jinsi ulivyo --Mungu wangu, Mfalme wangu, Mwokozi wangu--ninakuamini. Kwa sababu wewe ni muweza juu ya mbingu na nchi, ninasalimisha mapenzi yangu kwako, kila kitu changu. Chukua akili zangu, macho yangu, mdomo wangu, masikio yangu, moyo wangu, mikono yangu, na miguu yangu na uniongoze kwenye mapenzi yako. Ninakutumaini. Mungu, jibu langu ni ndiyo. Sasa, swali ni nini?”

Hebu fikiria kama uliomba namna hii. Unayachukia maombi ya usalama? Umechoka kuishi kwa mambo yasiyo ya maana? Unawadharau wakristo walio vuguvugu? Basi omba maombi ya hatari.

Mimi hapa, Bwana.

Nitume.

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Dangerous Prayers

Umechoka kujali usalama katika imani yako? Uko tayari kukabili hofu zako, kujenga imani yako, na kufikia uwezo wako kamili? Mpango huu wa Biblia wa siku 7 kutoka kwenye kitabu cha Mchungaji Craig Groeschel wa Life.Church, "Dangerous Prayers" yaani Maombi Hatari, unakujasiri uombe bila kujali usalama—kwa sababu kumfuata Yesu haukufaa kuwa salama salmini.

More

Tungependa kumshukuru Mchungaji Craig Groeschel na Life.Church kwa kutupa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea https://www.craiggroeschel.com/