Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maombi HatariMfano

Dangerous Prayers

SIKU 3 YA 7

Nichunguze

Unajaribu kuomba kwa njia ambayo hujawahi kuomba kabla?

Kwa moyo wako wote, roho, akili zako na nafsi yako yote? Kutatokea nini maishani mwako na maisha ya wale wote wanaokuzunguka kama utaanza kuomba maombi ya hatari?

Unajaribu kujua?

Mfalme Sauli kwa uongo alimshitaki Daudi kwa uhaini na kutuma jeshi lake lote kumtafuta Daudi mara kadha ili kuangamiza maisha yake. Kwa moyo wake wote, Daudi alitaka kumpendeza Mungu. Alipingana na hasira yake ili kulinda na kuonesha heshima kwa mfalme. Hali akijua nia yake siku zote haikuwa nzuri, Daudi aliusalimisha moyo wake mbele za Mungu na aliomba moja ya maombi magumu, ya wazi, na ya hatari ambayo hutaweza kuyasikia. Akitaka kumheshimu Mungu katika hali zote za maisha yake, Daudi aliomba “Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo yangu; Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, Ukaniongoze katika njia ya milele.” (Zab‬ ‭139:23-24‬)

Siyo tuu maombi haya ni magumu kuomba, lakini ni changamoto zaidi kuyatenda na kuyaishi. Kwa sababu kama una ujasiri kuyaomba, basi utahitaji kujizoeza kuishi kile Mungu atakujibu. Kwa hiyo usiombe kama humaanishi.

Nakuonya mapema, maombi haya yana uwezo wa kukuhukumu. Kukurekebisha. Kuyageuza maisha yako. Kubadilisha unavyojiona mwenyewe. Kubadirisha jinsi wengine wanavyokuona.

Yawezekana bado unafikiria kwamba hilo siyo tatizo. Yawezekana bado unajiuliza kwa nini umwambie Mungu auchunguze moyo wako wakati tayari yote yaliyo ndani yako. Unajua kuna nini.

Anajua kuna nini. Sasa kwa nini unaomba kitu kinachojulikana?

Hapo ndipo kwenye mtego. Kwa juu juu, inaonekana kama tunaweza kuijua mioyo yetu. Sawa? Ninajua nia zangu. Ninajua kilicho cha muhimu zaidi. Ninajua kwa nini ninafanya ninachokifanya. Zaidi ya hayo, unaweza kujiambia, Nina moyo mzuri. Sijaribu kuwaumiza watu. Nataka kufanya kilicho sahihi. Moyo wangu ni mzuri. Ninaomba, au siyo?

Lakini neno la Mungu ki ukweli linafunua kinyume chake. Inaweza kuwa ya kushtua unaposikia kwa mara ya kwanza, lakini Yeremia anatuambia ukweli waziwazi. Yeremia alikuwa mtoto wa kuhani wa kilawi aliyezaliwa 650 KK. Wakati wa utawala wa mfalme Yosia, Mungu alimuinua nabii huyu kijana kupeleka neno lake kwa Israeli na mataifa. Maneno ya Yeremia na yako--pamoja na mimi na kila mtu--hatuna mioyo mizuri. Kusema ukweli, siyo tuu moyo wako siyo mzuri, lakini moyo wako ni muovu na wenye dhambi katika hali zote. Nabii alisema, “Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?” (‭‭Yer‬ ‭17:9‬)

Pasipo Kristo, moyo wako ni mdanganyifu. Tunavyomkaribia Yesu, ndiyo tunavyoyaona mapungufu yetu. Kiburi. Ubinafsi. Tamaa. Ulevi. Roho ya kukashifu.

Kuomba maombi ya hatari yanaweza kufungua njia ya mawasiliano na Mungu. Badala ya kumwomba Mungu tuu afanye kitu kwa ajili yako, mwombe akufunulie kitu ndani yako. Wakati huu wa ukweli na Mungu unaweza usikubadirishe mara moja, lakini utakusaidia kutambua mahitaji yako ya kiroho na kuyaongoza maisha yako.

Ndiyo maana maombi haya ya Daudi ni ya hatari zaidi.

“Chunguza moyo wangu, Bwana.”

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Dangerous Prayers

Umechoka kujali usalama katika imani yako? Uko tayari kukabili hofu zako, kujenga imani yako, na kufikia uwezo wako kamili? Mpango huu wa Biblia wa siku 7 kutoka kwenye kitabu cha Mchungaji Craig Groeschel wa Life.Church, "Dangerous Prayers" yaani Maombi Hatari, unakujasiri uombe bila kujali usalama—kwa sababu kumfuata Yesu haukufaa kuwa salama salmini.

More

Tungependa kumshukuru Mchungaji Craig Groeschel na Life.Church kwa kutupa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea https://www.craiggroeschel.com/