Maombi HatariMfano
Funua Hofu Zangu
Ni kitu gani kinachokufanya uwe na shauku? wasiwasi? Kuhangaika? Kuogopa?
Sizungumzii uoga wa nje kama nyoka, buibui, au uoga wa kusafiri kwa ndege. Najiuliza ni kitu gani kinakufanya uwe macho usiku mzima, vitu vile vinavyojaa kwenye mawazo yako na kukataa kutulizwa. Vitu kama kupoteza kazi. Kutokuolewa au kuoa. Au kukwama katika ndoa mbaya. Kuwa na afya mbaya. Kwisha kwa akiba yako ya fedha za kujikimu.
Hatujui kwa uhakika sijui ni hofu gani zilikuwa kichwani mwa Daudi, lakini ni hakika kwamba alikuwa anasumbuliwa na usalama wake na yawezekana na maisha yake ya mbele. Kwa sababu baada ya kumwomba Mungu auchunguze moyo wake, Daudi aliomba, “uyajue mawazo yangu;” (Zab 139:23) Alitaka kushiriki hofu yake kuu na Mungu. Kukabiliana nazo na kuzipa majina. Kuamini kuwa Mungu ni mkuu kuliko hofu ambayo Daudi angeiwaza.
Uko tayari kuomba maombi kama hayo?“Bwana, funua kinachoteka mawazo yangu. Nioneshe hofu yangu kubwa. Endelea, nisaidie kukabiliana na vinavyonitisha.”
Tunavyoogopa ni muhimu.
Miaka iliyopita, nilipata ufunuo juu ya somo hili lililoniguza mimi binafsi. Mungu alinionesha kuwa kile ninachokiogopa sana kinaonesha jinsi navyomwamini Mungu kidogo. Baada ya kuzaliwa mtoto wetu wa tatu, Anna, Amy alianza kupata changamoto za mwili. Kwanza tulidhani ni uchovu tuu, lakini wakati nusu ya mwili wake kuanza kupata ganzi, tuliogopa itakuwa ni tatizo kubwa zaidi. Daktari mmoja baada ya mwingine hawakutoa majibu. Kwa kadri dalili zilivyozidi kuwa mbaya, imani yangu katika Mungu ilianza kudhoofika.
Hofu hii iliongeza nyingine, na usiku mawazo yalikuwa mengi. Itakuwaje kama Amy anaumwa sana? Itakuwaje kama nitampoteza? Sitaweza kulea watoto bila yeye. Sitaweza kuendelea kuliongoza kanisa. Sitapenda kuendelea. Nikapigwa sana. Vitu vilivyonifanya kukosa usingizi ni vitu ambavyo nilikuwa simwamini Mungu kwavyo. Nilikuwa navishikiria, kuvikumbatia, nikijaribu kuvitawala, kutatua matatizo yangu, kupanga kwa kila litakalotokea. Shukrani, kwa neema ya Mungu, Amy taratibu alianza kurejea kwenye hali yake, lakini changamoto yake ilinifunua katika udhaifu wangu mbaya zaidi. Hofu ilinitafuna.
Wewe je? Ni maeneo gani unayoyashikiria na kuyaruhusu yakutishe? Ni hofu gani unazomficha Mungu?
Fikiria. Kama umeshikwa na hofu kuhusu maisha ya baadaye ya ndoa, hii ni dalili kwamba humwamini kikamilifu Mungu kwa ndoa yako. Kama umeshikwa na hofu kwamba utalipaje bili zako, hii inaonesha kwamba yawezekana humwamini Mungu kama mpaji wako. Kama umeshikwa na hofu juu ya usalama wa watoto wako, yawezekana humwamini Mungu kuwatunza.
Mungu anapofunua hofu zako, atajenga pia imani yako. Unamhitaji. Unahitaji uwepo wake. Unahitaji nguvu yake. Unahitaji Roho wake kukuongoza. Unahitaji neno lake kukutia nguvu.
Kinachokutisha sana kinaonesha eneo ambalo unahitaji kukua na Mungu. Unaogopa nini? Wasiwasi wako ni nini?
Mungu anakuonesha nini?
Wapi unahitaji kukua katika imani?
Mwamini yeye.
Kuhusu Mpango huu
Umechoka kujali usalama katika imani yako? Uko tayari kukabili hofu zako, kujenga imani yako, na kufikia uwezo wako kamili? Mpango huu wa Biblia wa siku 7 kutoka kwenye kitabu cha Mchungaji Craig Groeschel wa Life.Church, "Dangerous Prayers" yaani Maombi Hatari, unakujasiri uombe bila kujali usalama—kwa sababu kumfuata Yesu haukufaa kuwa salama salmini.
More