Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 9Mfano

Soma Biblia Kila Siku 9

SIKU 9 YA 30

Bila Bwana kuwa Mwamba wao Waisraeli, je, mmoja angefukuzaje watu elfu, wawili wangekimbizaje elfu kumi?(m.30). Iliwezekana tu kwa mkono wa Bwana. Kuna uthibitisho mwingi wa ukweli huu: Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.… Israeli akamwacha Mungu aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake. … Israeli, humkumbuki Mwamba aliyekuzaa, Mungu aliyekuzaa umemsahau. … Mmoja angefukuzaje watu elfu, wawili wangekimbizaje elfu kumi, kama Mwamba wao asingaliwauza, kama Bwana asingaliwatoa? (Kum 32:4, 15, 18, 30). Bwana ni tofauti sana na ile miungu ambayo mataifa hujisifia kuwa ni mwamba wao (m.31-32:Mwamba wao si kama Mwamba wetu, hata adui zetu wenyewe ndivyo wahukumuvyo. Maana, mzabibu wao ni mzabibu wa Sodoma, nao ni wa mashamba ya Gomora; zabibu zao ni zabibu za uchungu, vichala vyao ni vichungu). Mwamba unamaanisha kitu kilicho imara ambacho hakitikishwi na jambo lolote. Mwamba wa Waisraeli ndiye aliyewaumba na kuwakomboa (m.15). Mwamba huo ndiye Kristo, kama ilivyoandikwa katika 1 Kor 10:4, Waisraeli waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo. Je, huyu ndiye Mwamba wa wokovu wako na kimbilio lako? 

siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 9

Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mithali

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz