Ingia katika KusudiMfano
Ingia katika Kusudi kupitia huduma ya Kujikana
Paulo anawataka Wagalatia kuishi maisha ya kujikana na kujitoa ambako kunakuwa tofauti na ulimwengu ulivyo. Uhuru tuliopokea kutoka kwa Kristo siyo kibali cha kuishi maisha ya ubinafsi, bali ni nafasi ya kumtukuza Mungu na kuwatumikia wengine kwa upendo (Angalia Wagalatia 5:13).
Tunaweza kumwangalia Yesu kama mfano halisi wa mtu aliyeingia katika kusudi lake kwa kujitoa. Katika unyenyekevu wake, alijua gharama ya kujitoa kama alivyosema, “Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke. Bado tunaona Yesu anafanya tendo kubwa la huduma ya kujitoa aliposema tena, “walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe”. Alikufa ili tuweze kuingia katika kusudi. alikufa ili tuweze kuwasaidia wengine kufanya hivyo hivyo(Angalia Mat 26:39).
Unapoomba, mwombe Bwana akufunulie kiwango unachoweza kuwasaidia wengine katika upendo. Unaweza kujikuta katika mazingira ambayo unawasaidia watu kanisani au kazini. Chochote unachofanya, fanya kama kwa Bwana kwa upendo na uhuru ambao amekwisha kupa.
Imeandikwa na Chenaniah Darma
Kama ungependa taarifa zaidi juu ya chuo cha C3, tafadhali ponyezahere.
Kuhusu Mpango huu
Kusudi langu ni nini? Ninatakiwa kufanya nini na maisha yangu? Mungu ana mpango gani kwa ajili yangu? Haya ndiyo maswali ambayo wengi wetu tunajiuliza katika maisha yetu. Tunakusudia kujibu baadhi ya maswali haya tunapofungua maana ya kuingia katika kusudi lako. Ungana na baadhi ya wanafunzi wetu wa C3 wanapotoa mwanga katika maudhui hii.
More