Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ingia katika KusudiMfano

Step into Purpose

SIKU 3 YA 5

Kusudi Lililorahisishwa

Wazo la "kusudi" ni jambo ambalo nilikuwa limenichanganya sana kuhusu kukulia kanisani.

Mungu alitakaje kunitumia? Nitajua lini? Nilitakiwa kufanya nini mpaka muda huo? Mara nyingi nilijiuliza maswali haya na kutoka kapa na kukata tamaa.

Hii ilikuwa ni jitihada ya kila siku mpaka siku moja nikapata andiko ambalo kusema ukweli lilinibadilisha maisha yangu-“Mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.” (1 Cor. 10:31)

Ufunuo umewekwa. 

Ndiyo, Mungu amefafanua mpango wa pekee kwa kila mmoja wetu. Ndiyo, kusudi lako ni tofauti na kusudi la kila mmoja. Lakini vitu vyote hivi vipo kwa ajili ya mmoja, kupindukia, kwa pamoja na kusudi la thamani: kuleta utukufu kwa Mungu.

Mungu hatafuti kuongeza majivuno! Wito wake wa kutukuzwa unatokana na upendo wake mkuu kwetu. Anajua kwamba tunapotambua uaminifu wake na kuweka thamani kwake, tunapokea ufunuo na kuanza kuuelewa upendo wake kwetu katika kiwango cha juu zaidi. Upendo huu hubadili kila kitu.

Mungu anatupenda tukimtukuza ama la, lakini shauku yake kwetu tujue ukamilifu wa upendo ule. Utukufu wote kwa Mungu! Hili ndilo kusudi letu.

 

Imeandikwa na Hannah White

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Step into Purpose

Kusudi langu ni nini? Ninatakiwa kufanya nini na maisha yangu? Mungu ana mpango gani kwa ajili yangu? Haya ndiyo maswali ambayo wengi wetu tunajiuliza katika maisha yetu. Tunakusudia kujibu baadhi ya maswali haya tunapofungua maana ya kuingia katika kusudi lako. Ungana na baadhi ya wanafunzi wetu wa C3 wanapotoa mwanga katika maudhui hii.

More

Tunapenda kulishukuru kanisa la C3 la Church Sydney Pty Ltd kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea https://www.c3college.com/