Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ingia katika KusudiMfano

Step into Purpose

SIKU 2 YA 5

Kusudi katika Kungoja 

Tunaishi katika kizazi cha Microwave. Kila kitu lazima kitokee sasa hivi. Hatuwezi kusubiri, na matokeo lazima yawe mara moja.Vivyo hivyo inaweza kuwa jinsi tunavyoona kusudi letu wakati mwingine.

Tunaweza kuamini kuwa Mungu anaweza kuwa ametuita kwa ajili ya kitu fulani- kuongoza maelfu kwenye ibada, kuwa na biashara inayokua na kupata mshahara wa tarakimu 6, kumpata mwenzi wa maisha yetu na kuoana, Kusafiri ulimwenguni ukihubiri injili...orodha inaendelea. Hakuna kosa kuamini mambo haya kutimia. Hata hivyo, mara nyingi inachukua muda na kusubiri ili kufikia mahali pale!

Inakadiriwa kwamba Daudi alikuwa na miaka 15 tu alipotiwa mafuta na Samweli ili kuwa mfalme wa Israeli, lakini Daudi hakuchukuwa nafasi hiyo mpaka alipotimiza miaka 30 (2 Samweli 5:4)! Katika miaka ile ya kusubiri, Mungu alimuandaa Daudi kuwa mfalme. Ilikuwa ni nyikani ambapo Daudi alijifunza baadhi ya mafundisho ya thamani sana ya maisha yake, ambapo alichoweza kukitegemea ni Mungu pekee.

Kusoma Zaburi kunatupa ufahamu wa huzuni alizozipitia. machozi aliyotoa, lakini pia jinsi alivyojifunza uaminifu wa Mungu, upendo wake mkuu na jinsi Daudi alivyoweza kupata nguvu na kimbilio ndani yake.Soma Zaburi 25. Katika kupitia nyakati hizi kulimfanya Daudi kuwa mkuu, mtu wa Mungu aliyechaguliwa kuwa mfalme wa Israeli.

Kama vile Daudi, Kipindi cha kusubiri kinaweza kisiwe chepesi, lakini ni kipindi ambacho Mungu hutuandaa kwa kila kilicho mbele tunapoingia kwenye kile alichonacho kwa ajili yetu! Kuwa na uhakika kwamba Mungu anaenda na wewe unapoingia katika mambo makubwa aliyokutayarishia.


Imeandikwa na Yoshua Sijl

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Step into Purpose

Kusudi langu ni nini? Ninatakiwa kufanya nini na maisha yangu? Mungu ana mpango gani kwa ajili yangu? Haya ndiyo maswali ambayo wengi wetu tunajiuliza katika maisha yetu. Tunakusudia kujibu baadhi ya maswali haya tunapofungua maana ya kuingia katika kusudi lako. Ungana na baadhi ya wanafunzi wetu wa C3 wanapotoa mwanga katika maudhui hii.

More

Tunapenda kulishukuru kanisa la C3 la Church Sydney Pty Ltd kwa kutoa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea https://www.c3college.com/