Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ninakujua. Ibada Kutoka Wakati wa NeemaMfano

I Know You: Devotions From Time of Grace

SIKU 4 YA 4

Najua upendo Wako na imani yako.

Wote tuna njaa ya kutambuliwa. Hebu kubali ukweli huo. Tunapofanya jambo vizuri au unamsaidia mtu, tunatarajia na tunatamani " Asante sana!" au " Wewe ni wa ajabu sana!" Kazi kubwa nyingi za imani, hata hivyo, zinafanywa na mashahidi wachache, au pasipokuwa na shahidi hata mmoja. Nani anaona masaa yanayochukua na mgonjwa wa kifafa? Nani anaona unapomtengenezea njia mama mjane jirani yako, unapomsaidia kodi shemeji yako ambaye hajui hesabu? Unapomnunulia mahitaji mtu ambaye hatoki nyumbani? Unapomfundisha mwanafunzi ambaye hawezi shuleni? Unapotumia saa nzima kwenye simu ukimshawishi rafiki anayetaka kujinyonga asifanye hivyo?

Mungu anafanya. Unaweza ukadhani anaona yote na kila mara unapomsaidia katika safari yake, uso wa Mungu unaonekana. Aliwaambia wakristo wa Thiatira “Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.” (‭‭Ufu.‬ ‭2:19‬) ‭


YesU alipoondoka duniani, alimtuma Roho wake kututia nguvu ili kutupandisha. Kimsingi alitupa kazi yake- kutangaza habari njema za injili na kutegemeza uadilifu wa ujumbe wenye uzima unaoaminika. Usijali kama huduma yako kwa watu wengine wakati mwingine inaonekana kama haionekani na haishukuriwi. Yeye unayempenda sana anafurahishwa sana na yale unayoyafanya.

Andiko

siku 3

Kuhusu Mpango huu

I Know You: Devotions From Time of Grace

Mungu alituumba kipekee. Na anajua huzuni zetu, furaha zetu, nguvu zetu, na udhaifu wetu.

More

Tulupenda kushukuru Huduma ya Muda wa Neema kwa kutupatia hii mpango. Kwa maelezo zaidi, atafathali nenda kwa: http://www.timeofgrace.org