Soma Biblia Kila Siku 5Mfano

Asafu, mtunzi wa zaburi hii, alimcha Mungu, tena aliongoza kwaya katika ukoo wa Walawi. Lakini ilimchanganya kuona waovu wakifanikiwa kuliko mtu wa Mungu. Hilo lilimfanya ajiulize maswali mengi. Jaribu hili lilitaka kumrudisha nyuma kiimani (m.2-3). Asafu alifikiri, wema wa Mungu ni kwa wacha Mungu na si vinginevyo (m.1). Tatizo la Asafu linatupata Wakristo wengi. Lakini leo tunafundishwa kuwa wema wa Mungu hauna mipaka (Baba yenu aliye mbinguni ... huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki; Mt 5:45). Sisi Wakristo tuwaombee mema wasiomcha Mungu ili wema wake uwavute wapate kutubu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 5 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/
Mipangilio yanayo husiana

Soma Biblia Kila Siku 12

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Soma Biblia Kila Siku 8

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021

Soma Biblia Kila Siku 9

Soma Biblia Kila Siku 11

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021

Soma Biblia Kila Siku 10

Uamuzi Mkubwa Zaidi wa Maisha Yako!
