Soma Biblia Kila Siku 5Mfano
Mungundiye awezaye kuokoa na kuangamiza, na jicho lake li kwao wamchao(Yak 4:12; Zab 33:18). Hawako peke yao, hata wapitapo hali ngumu. Kule motoni Mungu alikuweko. Aliingia pamoja na akina Danieli waliojitoa miili yao ili wasimtumikie mungu mwingine(m.28). Moto haukuwadhuru. Watesaji wao walishangaa, maana wasiomjua Mungu hawazijui nguvu zake ambazo kwazo huwalinda watu wake na kuwateketeza adui zake. Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza (Isa 43:2). Tafakari ahadi hii kutokana na habari za somo la leo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 5 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/