Soma Biblia Kila Siku 2Mfano
Yesu ni Mwokozi wa ulimwengu na ni mwalimu bora sana. Hapa ameketi akitoa mafundisho yanayopenya rohoni. Ghafla wajaribu wanaingilia kati! Lakini kwa neno moja Yesu anawafunulia unafiki na ujinga wao wa kutojua neno la Mungu. Pia anamwokoa yule mwanamke aliyesemwa kufumaniwa na washitaki wake. Kwa kumwonya yule mwanamke kutotenda dhambi tena na kuwanyamazisha washtaki wakatili, Yesu anajidhirisha kuwa Bwana na Mtawala wa Haki. Tulia na kumsikiliza Bwana Yesu kila siku.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 2 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Kitabu cha Kutoka na Injili ya Yohana, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz