Soma Biblia Kila Siku 2Mfano
Bwana, yeye umpendaye hawezi (m.3). Walimshirikisha Yesu matatizo yao. Nasi tufanye hivyo! Soma Wafilipi 4:6-7. Naye Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni ... ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo (m.4). Linganisha na Yn 9:1-3. Ugonjwa huu si wa mauti,maana yake ni kwamba bado ataendelea kuishi. Huu sio mwisho wa maisha yake. Wakati mwingine ugonjwa ni wa mauti, yaani, mwisho wa maisha ya mtu. Tunapoomba uponyaji tuseme "Mungu akipenda"!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 2 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Kitabu cha Kutoka na Injili ya Yohana, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz