Soma Biblia Kila Siku 2Mfano
Wayahudi hawakuelewa utumwa wao, Yesu alipowaambia kuwa kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi (m.34). Kisiasa walikuwa wanatawaliwa na Warumi, lakini walijua Yesu alizungumza juu ya hali yao ya kiroho. Hapo walijisifu kuwa wana wa Ibrahimu na watu wa Mungu. Kwa hiyo waliona hawajawahi kuwa watumwa. Lakini ni Yesu peke yake awezaye kutuweka huru kwelikweli! Kwa nini hawakumwelewa Yesu? Soma m.43! Kaa daima ndani ya neno la Yesu, maana ni la kweli na hutuweka huru kutoka utumwa wa dhambi.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 2 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Kitabu cha Kutoka na Injili ya Yohana, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz