Soma Biblia Kila Siku 2Mfano
Je, wewe unamfahamu Yesu kuwa nani? Ni jambo muhimu sana, maana ni hatua kuelekea kumwamini Yesu. Hapo haitoshi kuwa na elimu kubwa ya dini, maana tunaona viongozi wa kiyahudi hawakumfahamu Yesu kuwa yu nani. Jambo muhimu zaidi ni kusikiliza ushuhuda wa Yesu, maana unatusaidia kumwamini (m.30). Rudia kusoma m.12, 19 na 23, ukizingatia jinsi Yesu anavyojitambulisha hapo kwamba ni nuru ya ulimwengu, ni Mwana wa Mungu na ni Mwokozi wa ulimwengu. Tunapomwamini Yesu, hatutakufa katika dhambi zetu!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 2 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Kitabu cha Kutoka na Injili ya Yohana, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz