Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ipe Kazi Yako MaanaMfano

Give Your Work Meaning

SIKU 4 YA 4

Mungu Anatumia Kazi Yetu kwa Madhumuni Yake

Baada ya miaka mingi ya majaribu, ndoto za Yusufu zikatimika. Farao alimpa Yusufu mamlaka juu ya nchi yote ya Misri na ndugu zake wakaja kwake wakitafuta chakula wakati ambapo kulikuwa na ukame na kumwinamia ndugu yao, ingawa hawakumjua kama ni yeye papo hapo. Mungu alikusudia kutumia miaka saba ya shibe na miaka saba ya njaa tangu mwanzo kuongoza watu wake kwenda Misri ambapo wangepata kimbilio. Mungu alitumia mazingira kumtayarisha Yusufu kufanikisha mpango wake.

Yakobo alipofariki, ndugu zake Yusufu waliogopa kwamba angelipiza kisasi. Lakini Yusufu aliangalia madhumuni ya Mungu na kujibu, “Mlikusudia kunidhuru, lakini Mungu alikusudia mema […] kuokoa maisha ya watu wengi” (Mwanzo 50:20). Yusufu alipata kuona sehemu ndogo ya jinsi alivyopatana na mpango wa Mungu ambao ni mkuu kuliko tunavyoona leo. Siku moja, Yusufu ataona ni maisha mangapi alisaidia kuokoa. 

Yakobo 1:2-3 inatuambia, “Ndugu zangu, hesabuni kuwa ni furaha tupu mkiangukia katika majaribu mbalimbali, mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.” Tukiwa waaminifu katika magumu, tunamfungulia Mungu mlango kufanya mambo ya ajabu kupitia sisi. Ni muhimu kuamini kwamba Mungu ana uwezo na atatumia kazi yetu kukuza tabia, kutuimarisha, na hatimaye kuleta matokeo ambayo hayangetokea vinginevyo. 

Tukimwangalia Kristo, tunaweza kuwa na ujasiri kwamba Mungu anatumia kazi yetu zaidi kuliko tunavyofikiria. Pengine tutaona sehemu ndogo ya jinsi Mungu anavyotumia kazi yetu katika lengo lake kuu, kama Yusufu. Siku moja, sote tutapata fursa ya kuona mchango wa uaminifu wetu kwenye mpango wa Mungu. 

Jipe changamoto kumruhusu Mungu kukutakasa kupitia taabu, na kuinua maana ya kazi yako kwa madhumuni yake na utukufu wake.

Sala

Mungu Baba, najua kwamba daima u kazini ndani yangu na kupitia maisha yangu. Nisaidie kuzidi kuwa na mtazamo wa milele katika kazi ambayo ninafanya kila siku. Niongezee imani. Nipe hekima kazini mwangu ili kila kitu ambacho ninafanya kiweze kutumika kwa madhumuni yako. Katika jina la Yesu. Amina.

Kwa Uchunguzi Zaidi

Tazama mafunzo mengine kutoka Biblia kuhusu kazini kutoka Workmatters.

siku 3

Kuhusu Mpango huu

Give Your Work Meaning

Wengi wetu watatumia asilimia hamsini ya maisha yao kama watu wazima kazini. Tunataka kujua kwamba kazi yetu ina maana – kwamba kazi yetu ni muhimu. Lakini msongo, madai na taabu zinaweza kutufanya tufikiri kwamba kazi ni ngumu – kitu cha kuvumilia. Mpango huu utakusaidia kutambua nguvu ambayo unayo kuchagua maana chanya ya kazi yako ambayo ina msingi wa imani. 

More

Tungependa kushukuru Workmatters kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea:http://www.workmatters.org/workplace-devotions/