Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ipe Kazi Yako MaanaMfano

Give Your Work Meaning

SIKU 2 YA 4

Kuchagua Maana ya Mungu kuhusu Kazi

Mara nyingi, Wakristo wana fikra potofu kwamba kazi ambayo Mungu anaona kuwa muhimu ni kazi ya wachungaji, wamisionari na ya mashirika yasiyolenga kupata faida. Hii ni hatari kwa sababu tunaona kwamba kazi nyingine si ya maana, na unaweza kuwa na athari hasi kwa mtazamo na motisha wetu. Ukweli ni kwamba, kazi yote ni muhimu kwa Mungu. Mungu anataka tushirikiane naye katika kazi yoyote ambayo tunafanya ili tuwatumikie wengine na kutimiza matakwa yake.

Yusufu alielewa haya, hata katika majaribu yake makuu. Yusufu hakujenga mtazamo mbaya, hata mazingira yake ilivyozidi kuwa mabaya. Hakukubali tuu kazi hiyo kwa sababu haikuwa wito wake mkuu. Yuuefu alijua nani anamtumikia – Mungu. Matokeo yake, Mwanzo 39 inatuambia kwamba “Mungu alikuwa pamoja na Yusufu” mara nne (Mwanzo 39:2, 3, 21, 23). Mke wa Potifa alipoendelea kumwendea Yusufu, alisema “bwana wangu hajishughulishi na chochote nyumbani mwake. […] Nitawezaje … kumkosea Mungu?” Yusufu alitambua kwamba mafanikio yake yalitoka kwa Mungu na alihitaji kumheshimu kila wakati. 

Ingawa Yusufu alichagua kufanya kilicho sahihi, alishtakiwa bila hatia, akafukuzwa kazi, na kuwekwa gerezani. Hata katikati ya mazingira yasiyo haki, Yusufu hakuacha kumpa kumheshimu Mungu na kuwatumikia waliomzunguka. Tena, Mungu akampa kibali mbele ya mkuu wa gereza. 

Tutapitia mazingira yasiyo na haki kazini, kama Yusufu. Tunahitaji kujikinga kutokana na mtazamo hasi kwa kazi yetu mambo yanapoharibika. Yesu alituambia, “Ulimwenguni mnayo dhiki. lakini jipeni moyo! Mimi nimeushinda ulimwengu” (Yohana 16:33). Tunahitaji kuendelea kukaa ndani ya Kristo katika hali zote, na kazi yetu itazaa matunda mengi (Yohana 15:5). 

Utafanyaje ili utazame kazi yako kupitia macho ya Mungu leo? 

Sala

Mungu Baba, nasema asante kwa kazi ambayo umenipa. Asante kwa kunipa mafanikio. Nisaidie kukaa ndani yako nyakati zote ili niweze kuwahudumia wengine kwa uhodari katika hali zote, hata iwapo mambo yananiendea mrama. Nisaidie kumwangalia Yesu. Katika jina la Yesu. Amina.

Kwa Uchunguzi Zaidi

Gundua jinsi ya kutafuta kusudi la Mungu kwa kazi. Tazama video hii ya Bonnie Wurzbacher , Makamu wa Rais wa zamani (SVP), Kampuni ya Coca-Cola.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Give Your Work Meaning

Wengi wetu watatumia asilimia hamsini ya maisha yao kama watu wazima kazini. Tunataka kujua kwamba kazi yetu ina maana – kwamba kazi yetu ni muhimu. Lakini msongo, madai na taabu zinaweza kutufanya tufikiri kwamba kazi ni ngumu – kitu cha kuvumilia. Mpango huu utakusaidia kutambua nguvu ambayo unayo kuchagua maana chanya ya kazi yako ambayo ina msingi wa imani. 

More

Tungependa kushukuru Workmatters kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea:http://www.workmatters.org/workplace-devotions/