Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ipe Kazi Yako MaanaMfano

Give Your Work Meaning

SIKU 3 YA 4

Kumtegemea Mungu Nyakati Zote

Tunayemfanyia kazi inajalisha sana na kuathiri umuhimu wa kazi hiyo. Ikiwa tunawaheshimu watu ambao tunafanyia kazi na kupenda shirika letu, ni wazi kwamba tutataka kufanya kazi bora zaidi. Lakini tunaponyanyaswa, ama tukizozana na wenzetu kazini, ni rahisi kuvunjika moyo, kufadhaishwa ama hata kukasirika. Maoni yetu kuhusu watu yanaweza kuathiri motisha ya kufanya kazi bora zaidi. 

Yusufu alikuwa na kila sababu ya kuwa na hasira na uchungu. Alitupwa gerezani kwa kosa asilolitenda. Hata hivyo, Yusufu aliendelea kumtegemea Mungu na kumtumikia mkuu wa gereza kwa uhodari. Kwa sababu hiyo, akafanywa msimamizi wa wafungwa wote. Mwokaji na mnyweshaji, ambaye alitumwa huko, alionekana kuwa na huzuni, Yusufu alionyesha kujali. Aliwasikiliza wakimfafanulia ndoto zao za kutisha na kutoa tafsiri ambayo Mungu alimwonyesha. Wema wake ulimfanya mnyweshaji kumpendekeza Yusufu kwa Farao baada ya Farao kuwa na ndoto ambayo hakuna aliyeweza kutafsiri. Hata hivyo, Yusufu hakujigamba. Alimwambia Farao kwamba hakuna anayeweza kutafsiri ndoto ila Mungu. Kisha akatoa tafsiri ambayo Mungu alimpa. 

Kwa kuwa Yusufu alikuwa mwaminifu gerezani, Mungu alimpa mamlaka juu ya nchi yote ya Misri (Luka 16:10). Mungu alikuwa pamoja na Yusufu siku zote, akimtayarisha, akimpa hekima na akipanga mazingira ili atimize makusudi yake. 

Ikiwa motisha yetu ya kufanya kazi bora inaathiriwa na tabia za wengine, msimamo wetu wa kufanya vizuri utayumbayumba. Lakini ingekuwaje kama daima ungemtegemea Mungu kazini mwako? Kufanya kazi yetu kwa sababu Mungu unatuwezesha, siku zote, kupata matokeo bora. Unaweza kuongeza kumtegemea kwako Mungu kazini kwako leo?

Sala

Baba, nisamehe kwa nyakati ambazo nimeruhusu maoni yangu kuhusu watu kupotosha mtazamo wangu wa kazi yangu. Niongezee imani ya kwamba utatumia kazi yangu yote kukupa heshima daima. Fanya kazi moyoni mwangu ili nizidi kuwa na mtazamo chanya. Katika jina la Yesu. Amina.

 

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Give Your Work Meaning

Wengi wetu watatumia asilimia hamsini ya maisha yao kama watu wazima kazini. Tunataka kujua kwamba kazi yetu ina maana – kwamba kazi yetu ni muhimu. Lakini msongo, madai na taabu zinaweza kutufanya tufikiri kwamba kazi ni ngumu – kitu cha kuvumilia. Mpango huu utakusaidia kutambua nguvu ambayo unayo kuchagua maana chanya ya kazi yako ambayo ina msingi wa imani. 

More

Tungependa kushukuru Workmatters kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea:http://www.workmatters.org/workplace-devotions/