Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Oswald Chambers: Furaha- Nguvu katika BwanaMfano

Oswald Chambers: Joy - Strength In The Lord

SIKU 2 YA 30

Baraka za Mungu zinaanguka, kama mvua yake, kwa waovu na wazuri sawia. Baraka kuu za afya, werevu, mafanikio, zote zatoka neema yake yanayofurika, wala si tabia ya wanaopokea. Kwa mfano, ikiwa afya nzuri ingekuwa ishara kwamba mtu ni mtakatifu, tungepoteza uwezo wa kutambua tabia njema, kwani watu wabaya wengi wana afya nzuri.

Kuna tofauti kati ya mazingira na hali. Kila mtu ana mazingira yake mwenyewe; ni hiyo sehemu ya hali yake inayoafikiana na hulka yake. Tunaunda mazingira yetu wenyewe, hulka yetu inatuundia mazingira haya. Raha inamaanisha kwamba tunachagua tu vitu katika hali yetu vinavyotufurahisha. Ni msingi bora wa Ukristo bandia. Hakuna mahali kumeandikwa katika Biblia kuhusu Mkristo "mwenye raha”; furaha imezungumziwa mara nyingi. Raha inategemea vitu vinavyotendeka. Vitu vya nje haviathiri furaha.

Maswali ya Kutafakari: Shida inaathiri furaha yangu vipi? Ninapima upendo wa Mungu kwangu kupitia baraka zake kwangu?

Dondoo zimetoka "God’s Workmanship" na "The Shadow of an Agony", © Discovery House Publishers

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Oswald Chambers: Joy - Strength In The Lord

Gundua hekima ya Oswald Chambers, mwandishi wa "My Utmost for His Highest", katika mkusanyiko huu wa hazina ambao unatoa ufahamu kuhusu furaha. Kila somo lina dondoo kutoka Chambers na maswali ya kutafakari kibinafsi. Akitumia hekima sahili na dhahiri kutoka Biblia kukupa motisha na changamoto, utaanza kutamani kuwasiliana zaidi na Mungu.

More

We would like to thank Discovery House Publishers for providing this plan. For more information, please visit: www.utmost.org