Zaburi 41:4-6
Zaburi 41:4-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nami nilisema, BWANA, unifadhili, Uniponye roho yangu maana nimekutenda dhambi. Adui zangu wananitaja kwa maneno mabaya, Atakufa lini, jina lake lipotee? Na mmoja wao akija kunitazama asema uongo, Moyo wake hujikusanyia maovu, Naye atokapo nje huyanena.
Zaburi 41:4-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nilisema, “Ee BWANA nihurumie, niponye, maana nimekutenda dhambi wewe.” Adui zangu wanasema kwa hila, “Lini atakufa, na jina lake litokomee kabisa.” Kila anapokuja mtu kunitazama, huzungumza uongo, huku moyo wake hukusanya masingizio; kisha huondoka na kuyasambaza huku na huko.
Zaburi 41:4-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Nami nilisema: “Unifadhili, ee Mwenyezi-Mungu, unihurumie maana nimekukosea wewe.” Madui zangu husema vibaya juu yangu: “Atakufa lini na jina lake litoweke!” Wanitembeleapo husema maneno matupu; wanakusanya mabaya juu yangu, na wafikapo nje huwatangazia wengine.
Zaburi 41:4-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nami nalisema, BWANA, unifadhili, Uniponye roho yangu maana nimekutenda dhambi. Adui zangu wananitaja kwa maneno mabaya, Atakufa lini, jina lake likapotea? Na mmoja wao akija kunitazama asema uongo, Moyo wake hujikusanyia maovu, Naye atokapo nje huyanena.