Mwanzo 31:44-49
Mwanzo 31:44-49 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Haya! Na tufanye agano, mimi na wewe, liwe kwa ushahidi kati ya mimi na wewe. Yakobo akatwaa jiwe akalisimamisha kama nguzo. Yakobo akawaambia ndugu zake, Kusanyeni mawe. Wakatwaa mawe, wakafanya chungu, nao wakala huko karibu na ile chungu. Labani aliiita Yegarsahadutha, lakini Yakobo aliiita Galedi. Labani akasema, Chungu hii ni shahidi kati ya mimi na wewe hivi leo. Kwa hiyo likaitwa jina lake Galedi, na Mispa, maana alisema, Mungu avizie kati ya mimi na wewe, wakati tusipoonana.
Mwanzo 31:44-49 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Haya! Na tufanye agano, mimi na wewe, liwe kwa ushahidi kati ya mimi na wewe. Yakobo akatwaa jiwe akalisimamisha kama nguzo. Yakobo akawaambia ndugu zake, Kusanyeni mawe. Wakatwaa mawe, wakafanya chungu, nao wakala huko karibu na ile chungu. Labani aliiita Yegarsahadutha, lakini Yakobo aliiita Galedi. Labani akasema, Chungu hii ni shahidi kati ya mimi na wewe hivi leo. Kwa hiyo likaitwa jina lake Galedi, na Mispa, maana alisema, Mungu avizie kati ya mimi na wewe, wakati tusipoonana.
Mwanzo 31:44-49 Biblia Habari Njema (BHN)
Basi, tufanye agano mimi nawe, liwe ushahidi kati yako nami.” Basi, Yakobo akachukua jiwe, akalisimika kama nguzo ya ukumbusho. Tena Yakobo akawaambia ndugu zake, “Kusanyeni mawe.” Nao wakakusanya mawe na kufanya rundo. Kisha wakala chakula karibu na rundo hilo la mawe. Labani akaliita rundo hilo Yegar-sahadutha, lakini Yakobo akaliita Galeedi. Labani akasema, “Rundo hili ni ushahidi kati yako na mimi leo.” Kwa hiyo Labani akaliita Galeedi, na ile nguzo akaiita Mizpa akisema, “Mwenyezi-Mungu na atulinde tuwapo mbali bila kuonana.
Mwanzo 31:44-49 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Njoo sasa na tufanye agano, wewe na mimi, na liwe kama shahidi kati yetu.” Hivyo Yakobo akachukua jiwe, akalisimamisha kama nguzo. Akawaambia jamaa yake, “Kusanyeni mawe.” Hivyo wakachukua mawe na kuyakusanya yakawa lundo, wakala chakula hapo karibu na hilo lundo. Labani akaliita Yegar-Sahadutha na Yakobo akaliita Galeedi. Labani akasema, “Lundo hili ni shahidi kati yako na mimi leo.” Ndiyo maana likaitwa Galeedi. Pia liliitwa Mispa, kwa sababu alisema, “BWANA na aweke ulinzi kati yako na mimi wakati kila mmoja akiwa mbali na mwingine.