Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 31:44-49

Mwanzo 31:44-49 SRUV

Haya! Na tufanye agano, mimi na wewe, liwe kwa ushahidi kati ya mimi na wewe. Yakobo akatwaa jiwe akalisimamisha kama nguzo. Yakobo akawaambia ndugu zake, Kusanyeni mawe. Wakatwaa mawe, wakafanya chungu, nao wakala huko karibu na ile chungu. Labani aliiita Yegarsahadutha, lakini Yakobo aliiita Galedi. Labani akasema, Chungu hii ni shahidi kati ya mimi na wewe hivi leo. Kwa hiyo likaitwa jina lake Galedi, na Mispa, maana alisema, Mungu avizie kati ya mimi na wewe, wakati tusipoonana.

Soma Mwanzo 31

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mwanzo 31:44-49