Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwa 31

31
Yakobo Atoroka na Jamaa na Mifugo yake
1 # Ayu 5:2; 31:31; Zab 57:4; Rum 13:13; Tit 3:3; Yak 3:8; Zab 49:16 Basi Yakobo akasikia maneno ya wana wa Labani, wakisema, Yakobo amechukua mali yote ya baba yetu; na kwa mali ya baba yetu amepata fahari hii yote. 2#Mwa 4:5; Kum 28:54Yakobo akaona uso wa Labani, ya kuwa hakumtazama vema kama jana na juzi. 3#Mwa 28:15; 32:9BWANA akamwambia Yakobo, Urudi mpaka nchi ya baba zako na kwa jamaa zako, nami nitakuwa pamoja nawe. 4Yakobo akatuma watu, akawaita Raheli na Lea waje nyikani kwenye wanyama wake. Akawaambia, 5#Mwa 21:22; Isa 41:10; Ebr 13:5Naona uso wa baba yenu, kwamba hanitazami vema kama jana na juzi. Lakini Mungu wa baba yangu amekuwa pamoja nami. 6#Mwa 30:29Nanyi mmejua ya kwamba kwa nguvu zangu zote nimemtumikia baba yenu. 7#Mwa 15:1; 20:6; Ayu 22:25; Zab 5:11; 7:10; Mit 30:5Na baba yenu amenidanganya, akabadili mshahara wangu mara kumi; lakini Mungu hakumwacha kunidhuru. 8#Mwa 30:32Aliposema, Walio na madoadoa watakuwa mshahara wako, wanyama wote wakazaa madoadoa. Aliposema, Walio na milia watakuwa mshahara wako, ndipo wanyama wote wakazaa wenye milia. 9#Mwa 31:16Hivi Mungu akamnyang’anya mali yake baba yenu, na kunipa mimi. 10Ikawa, wakati wale wanyama walipochukua mimba, naliinua macho yangu nikaona katika ndoto, na tazama, mabeberu waliowapanda hao wanyama walikuwa na milia, na madoadoa, na marakaraka. 11#Mwa 48:16Na malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, Yakobo! Nikasema, Mimi hapa. 12#Kut 3:7; Kum 24:15; Zab 12:5; Efe 6:9Akasema, Inua, basi, macho yako, ukaone; mabeberu wote wanaopanda wanyama wana milia, na madoadoa, na marakaraka; maana nimeona yote aliyokutendea Labani. 13#Mwa 28:18-22; 32:9Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa. 14#Mwa 2:24Raheli na Lea wakajibu, wakamwambia, Je! Imetubakia sehemu au urithi katika nyumba ya baba yetu? 15#Amu 17:5; 1 Sam 19:13; Eze 21:21; Hos 3:4Hakutufanya kama wageni, maana ametuuza, naye amekula fedha zetu kabisa? 16Maana mali yote ambayo Mungu amemnyang’anya baba yetu, mali hiyo ndiyo yetu na ya wana wetu. Basi yo yote Mungu aliyokuambia, uyafanye.
17Ndipo Yakobo akaondoka, akapandisha wanawe na wakeze juu ya ngamia. 18Akachukua wanyama wake wote, na mali yake yote aliyokuwa ameyapata, na wanyama aliowapata katika Padan-aramu, ili afike kwa Isaka babaye katika nchi ya Kanaani. 19#Mwa 35:2Basi Labani alikuwa amekwenda kuwakata manyoya kondoo zake, na Raheli akaviiba vinyago vya babaye. 20Yakobo akamhadaa Labani, Mshami, kwa kuwa hakumwambia ya kwamba anakimbia. 21#Mwa 46:28; 2 Fal 12:17; Lk 9:51Basi akakimbia yeye na yote aliyokuwa nayo; akaondoka akauvuka mto, akaelekeza uso wake kwenda mlima wa Gileadi.
Labani Amfuatilia Yakobo
22Hata siku ya tatu Labani akaambiwa ya kwamba Yakobo amekimbia, 23#Mwa 13:8akatwaa ndugu zake pamoja naye, akamfuata mwendo wa siku saba. Akampata katika mlima wa Gileadi. 24#Mwa 20:3; Ayu 33:15; Mt 1:20; Mwa 24:50Mungu akamjia Labani, Mshami, katika ndoto ya usiku, akamwambia, Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari.
25Labani akamfikia Yakobo, na Yakobo alikuwa amepiga hema zake katika mlima, na Labani na ndugu zake wakapiga hema zao katika mlima wa Gileadi. 26#1 Sam 30:2Labani akamwambia Yakobo, Umefanya nini? Umenihadaa, ukawachukua binti zangu kama mateka waliotwaliwa kwa upanga. 27Mbona umekimbia kwa siri ukanihadaa, wala hukuniambia, nipate kuagana nawe uende zako kwa furaha, na nyimbo, na ngoma, na kinubi? 28#Rut 1:9; 1 Fal 19:20; Mdo 20:37; 1 Sam 13:13; 2 Nya 16:9Wala hukuniacha niwabusu wanangu, na binti zangu; basi umetenda upumbavu. 29#Mwa 28:13; Zab 5:11; 84:11; 115:9Ninao uwezo mkononi mwangu wa kukufanyia madhara; lakini Mungu wa baba yako usiku huu ameniambia, akisema, Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari. 30#Mwa 31:19; Yos 24:2; Amu 18:24; Mdo 19:26Basi sasa, umetoka kwa sababu umetamani sana nyumba ya baba yako. Mbona basi umeiiba miungu yangu?
31Yakobo akajibu, akamwambia Labani, Kwa sababu naliogopa, nikasema, Usije ukaninyang’anya binti zako kwa nguvu. 32#Mwa 44:9Awaye yote utakayemwona kuwa nayo miungu yako, yeye asiishi. Mbele ya ndugu zetu ukitambue kilicho chako kwangu, ukakichukue. Maana Yakobo hakujua ya kwamba Raheli ameiiba. 33#Mwa 44:9Labani akaingia katika hema ya Yakobo, na hema ya Lea, na hema ya vijakazi wawili, wala hakuiona. Akatoka katika hema ya Lea, akaingia katika hema ya Raheli. 34Basi Raheli alikuwa amevitwaa vile vinyago ameviweka katika matandiko ya ngamia, na kuvikalia. Labani akapapasa hema yote wala hakuviona. 35#Kut 20:12; Law 19:32; Efe 6:1Naye Raheli akamwambia babaye, Bwana wangu asikasirike kwa sababu siwezi kuinuka mbele yako, maana nimeshikwa na mambo ya kike. Akatafuta, wala hakuviona vile vinyago.
36 # Efe 4:26 Yakobo akakasirika, akagombana na Labani. Yakobo akajibu, akamwambia Labani, N’nini hatia yangu? Nayo ni nini dhambi yangu, hata ukanifuatia namna hii? 37#1 Sam 12:3; 1 Kor 6:5Umepapasa-papasa vyombo vyangu vyote; ni kitu gani ulichokiona cha nyumbani mwako? Kiweke hapa mbele ya ndugu zangu, na ndugu zako, wakaamue kati yetu. 38Miaka hii ishirini nimekaa kwako; kondoo zako wala mbuzi zako wake hawakuharibu mimba wala waume katika wanyama wako sikuwala. 39#Kut 22:10,12Kilichoraruliwa na hayawani sikukuletea, mimi mwenyewe nimetwaa hasara yake, wewe umekidai katika mkono wangu, ikiwa kilichukuliwa mchana, au ikiwa kilichukuliwa usiku. 40Hii ilikuwa hali yangu; mchana jua likanipata, na baridi usiku, usingizi ukanitoka machoni mwangu. 41#Mwa 29:27; 31:7Miaka hii ishirini nimekaa nyumbani mwako; nilikutumikia miaka kumi na minne kwa binti zako wawili, na miaka sita kwa wanyama wako, nawe umebadili mshahara wangu mara kumi. 42#Zab 124:1; Isa 8:13; Kut 3:7; 1 Nya 12:17Kama Mungu wa baba yangu, Mungu wa Ibrahimu na Hofu ya Isaka, hangalikuwa pamoja nami, hakika sasa ungalinifukuza mikono mitupu. Mateso yangu na kazi za mikono yangu Mungu ameziona, akakukemea usiku huu.
Labani na Yakobo Wawekeana Agano
43Labani akajibu, akamwambia Yakobo, Hao binti ni binti zangu, na wana ni wanangu, na wanyama ni wanyama wangu, na yote uyaonayo ni yangu; nami naweza kuwatendea nini leo binti zangu na wana wao waliowalea? 44#Mwa 26:28; Yos 24:27Haya! Na tufanye agano, mimi na wewe, liwe kwa ushahidi kati ya mimi na wewe.
45 # Mwa 28:18 Yakobo akatwaa jiwe akalisimamisha kama nguzo. 46Yakobo akawaambia ndugu zake, Kusanyeni mawe. Wakatwaa mawe, wakafanya chungu, nao wakala huko karibu na ile chungu. 47Labani aliiita Yegarsahadutha, lakini Yakobo aliiita Galedi. 48#Yos 24:27Labani akasema, Chungu hii ni shahidi kati ya mimi na wewe hivi leo. Kwa hiyo likaitwa jina lake Galedi, 49#Amu 11:29; 1 Sam 7:5na Mispa, maana alisema, Mungu avizie kati ya mimi na wewe, wakati tusipoonana. 50Ukiwatesa binti zangu, na ukitwaa wake zaidi ya binti zangu, wala hapana mtu pamoja nasi, tazama, Mungu ni shahidi kati ya mimi na wewe. 51Labani akamwambia Yakobo, Tazama chungu hii utazame na nguzo niliyoitia kati ya mimi na wewe. 52Chungu hii na iwe shahidi, na nguzo hii na iwe shahidi, ya kuwa mimi sitapita chungu hii kuja kwako, wala wewe hutapita chungu hii na nguzo hii uje kwangu, kwa madhara. 53#Mwa 16:5; 21:23Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Nahori, Mungu wa baba yao, ahukumu kati yetu.
Yakobo akaapa kwa Hofu ya Isaka baba yake. 54Yakobo akachinja sadaka katika mlima, akawaita ndugu zake waje wale chakula, nao wakala chakula, wakakaa usiku kucha mlimani. 55#Mwa 28:1; 2 Sam 6:20Labani akaondoka asubuhi na mapema, akawabusu wanawe na binti zake, akawabariki; kisha Labani akaenda zake, akarudi kwao.

Iliyochaguliwa sasa

Mwa 31: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia