Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 77:9-13

Zaburi 77:9-13 BHN

Je, Mungu amesahau kuwa na huruma? Je, hasira yake imeuondoa upole wake?” Kisha nikasema, “Kinachonichoma zaidi ni kwamba, Mungu Mkuu hatendi tena kitu kwa ajili yetu!” Nitayakumbuka matendo yako, ee Mwenyezi-Mungu, naam, nitayafikiria maajabu yako ya hapo kale. Nitatafakari juu ya kazi zako, na kuwaza juu ya matendo yako makuu. Kila ufanyacho ee Mungu, ni kitakatifu. Ni mungu gani aliye mkuu kama Mungu wetu?

Soma Zaburi 77